Viongozi na wananchi wa Wilaya ya Ruangwa wametoa maoni yao kuhusu Mradi wa kuboresha upatikanaji wa huduma za maji vijijini kwa ubia kati ya Serikali na Sekta binafsi.
Maoni hayo yametolewa katika Warsha iliyofanyika leo Mei 21, 2024 katika Ukumbi wa mikutano wa Mkuu wa Wilaya, hii ni kufuatia mpango mkakati wa Wizara ya Maji kuona umuhimu wa kuboresha huduma ya maji na usafi wa Mazingira vijijini.
Serikali kupitia Wizara ya Maji ina lengo ifikapo 2025 wananchi vijijini wawe wamepatiwa huduma ya maji kwa asilimia 85 na ifikapo 2030 iwe imefikia asilimia 100 na ili kufikia lengo hilo ni muhimu kushirikisha Sekta binafsi kwa kuzingatia maslahi ya wananchi vijijini na si mwekezaji pekee ili kuondoa sintofahamu.
Utekelezaji wa Mradi huu umeshirikisha Mikoa Mitano ya Kanda ya Mashariki ambayo ni Lindi, Mtwara, Pwani, Dar es salaam na Morogoro na kwa Mkoa wa Lindi Wilaya zilizopendekezwa na Serikali kukusanya maoni ya wananchi kuhusu mradi wa kuboresha huduma za maji vijijini ni Wilaya ya Lindi, Kilwa na Ruangwa.
Kwa upande wake Mratibu wa Vyombo vya utoaji huduma ya maji ngazi ya jamii Mkoa wa Lindi Ndugu Rogers Baijuki amewashukuru viongozi na wananchi wa Wilaya ya Ruangwa kwa utoaji wa maoni kuhusu mradi husika halikadhalika amewaomba kutoa ushirikiano kwa Kampuni ya Disney International ambayo itakuja kufanya upembuzi yakinifu ili kujiridhisha kwa kina namna bora ya ufanyaji wa mradi bila kuleta changamoto kwa Serikali, wawekezaji na mamlaka zilizopewa jukumu la kusimamia mradi huo.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa