Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Mhe. Andrew Chikongwe, ametangaza kwa furaha kwamba vijiji vyote 90 vya Wilaya ya Ruangwa sasa vina umeme, ameyasema hayo Leo, Julai 29, 2024 akiwa katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Mkuu wa Wilaya, alipokuwa akichangia maoni kwenye kongamano la ukusanyaji wa maoni ya Dira ya Taifa ya maendeleo ya mwaka 2050.
Aidha,Mhe. Chikongwe ameeleza kuwa hatua hii ni muhimu kwa maendeleo ya jamii na ametoa shukrani za dhati kwa Serikali kwa kutekeleza mradi huu mkubwa ambao utaongeza fursa za kiuchumi, elimu, na afya kwa wananchi. Umeme huo utachangia kuboresha hali ya maisha na kuleta maendeleo endelevu katika Wilaya ya Ruangwa.
Hatua hii inawakilisha mwanzo wa mapinduzi makubwa katika maisha ya wananchi wa Ruangwa, ikiwa ni hatua muhimu katika kuimarisha maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika eneo hilo.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa