Akizungumza wakati walipotembelea ujenzi wa uwanja huo na kuona vijana walioamua kufyatua tofali kwa kujitolea uwanjani hapo, Mwenyekiti wa ALAT Mkoani Lindi ambae pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya WIlaya Ruangwa mh. Rashid Nakumbya amewashukuru vijana hao kwa kujitoa katika shughuli za kimaendeleo na kusisitiza kuwa kwa sasa wana Ruangwa na Lindi kwa jumla tunazungumza lugha moja ya maendeleo na si vinginevyo.
Nakumbya ameleeza kuwa Mkoa wa lindi ni miongoni mwa Mkoa ambayo inatajwa kuwa nyuma kimaendeleo na hivyo kueleza kuwa katika vikao vyao (ALAT) Mkoa wamekua wakihakikisha wanapambana na kuweka mikakati ya kuhakikisha mkoa huo unatoka nyuma na kusogea mbele.
“ na katika kusogea mbele hakuna ubaguzi ndio maana wako hapa leo na wote wanaunga mkono maendeleo, na ni imani yangu vijana watatumika zaidi kuhamasisha maendeleo katka maeneo yao” alisema, nakumbya wakati akizungumza na vijana pamja na wajumbe waliofika kutembelea uwanja huo.
Naye Katibu wa vijana walijitolea kufyatua tofali kwa ajili ya ujezi wa ukuta wa uwanja huo bw.Ibrahim Joshua, amesema wameamua kuhamasisha vijana kutoka vijiji vyote wilayani humo na kukubali kujitolea kufika uwanjani hapo kuendesha shughuli ya awali ya ufyatuaji tofali kwa ajili ya ujenzi wa ukuta wa uwanja huo wa kisasa unaotegemewa kukamilika mwishoni mwa mwezi wa saba.
Amesema awali kambi yao ilipangwa kumalizika kwa muda wa siku saba lakini kutokana na umuhimu wake kuonekana bado vijana walikua na hari wakaongeza siku mbili ili kukamilisha ili kumalizia idadi ya mifuko ya sementi iliyokuwapo uwanjani hapo.
“vijana wapo tayari kutumikia jambo hili siku yeyote, na ndiyo maana leo ndio siku ya mwisho ya awamu ya kwanza ya kujitoa kwa ajili ya ujenzi huu kwa maana ya kwamba kufyatua tofali, lakini jumapili tunarud tena kwahiyo ni ishara kwamba vijana hawa wamejitoa kwa moyo wao thabiti” amesema ibrahim.
Aidha kwa upande wa wajumbe wa (ALAT) Lindi walifika kutembelea mradi huo wa ujenzi wa uwanja, wamefurahishwa kwa kuona vijana hao wamejitoa kwa ajili ya kufanikisha ufyatuaji wa tofali kwa ajili ya ujenzi wa uwanja huo bila malipo, huku wakieleza kuwa jambo hilo linasogeza kasi ya maendeleo na kusema kuwa ni jambo la kujifunza na kuiga kwa kujivunia.
Jumla ya mifuko ya sementi 422(mia nne ishirini na mbili) iliozalisha tofali 7871 (elfu saba mia nane sabini na moja) imefyatuliwa na vijana hao ambao wameweka kambi uwanjani hapo kwa muda wa siku tisa ili kusaidia kuongeza kasi ya kufanikisha kukamilika kwa ujenzi wa kuta za uwanja huo. Uwanja huo unaendelea kujengwa wilayani ruangwa ambao umepewa jina la majaliwa vibrant play ground unategemewa kukamilika mwishoni mwa mwezi wa saba mwaka huu ili mwanzoni mwa mwez wa nane uanze kutumika kwa kutimua kivumb katika mashindano la ligi daraja la kwanza Nchini.
Mwisho
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa