Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Mw. George Mbesigwa amewataka washiriki wa mafunzo ya ufugaji kuku na samaki kwenda kutekeleza mafunzo hayo kwa vitendo na pia kuwarithisha wananchi wengine ujuzi mliopata.
Aliyasema hayo wakati akifunga mafunzo ya siku tano yaliyofanyika katika chuo cha VETA cha wilaya ya Ruangwa ambapo jumla ya washiriki 264 kutoka kata 9 walinufaika na mafunzo hayo. Kata hizo ni Nandagala, Malolo, Likunja, Ruangwa, Nachingwea, Namahema, Chienjere, Nkowe na Mnacho
VETA imekuwa ikitoa mafunzo hayo kupitia mfumo uitwao (INTEP Integrated Training for Entrepreneurship Promotion) ikiwa lengo ni kuandaa na kujengea uwezo wajasiliamali wadogo ili waweze kukua na kuongeza ufanisi na tija katika biashara zao na hatimae kuongeza kipato katika ngazi ya familia, jamii na taifa kwa ujumla.
"Mafunzo haya yangeweza kupelekwa sehemu nyingine ila yameletwa Ruangwa hivyo ni wajibu wenu kuyafanya mafunzo haya kuwa endelevu, nendeni mkafuge kuku na samaki kama ulivyofunzwa" amesema Mbesigwa
Pia aliwataka washiriki kuendeleza elimu na ujuzi waliopata katika mafunzo na kwa sababu mshiriki anaweza kufuga kuku na samaki na akaendelea kufanya shughuli nyingine za kujiongezea kipato lakini pia kukidhi kiu ya uhitaji ya wana Ruangwa.
Aidha aliuomba uongozi wa VETA Kanda ya Kusini Mashariki kuhakikisha kuwa Kata 13 zilizobaki zinapatiwa mafunzo kama haya au mengineyo ili kuisaidia jamii yote kujikomboa kiuchumi.
Kuhusu mafunzo katika chuo cha VETA cha wilaya ya Ruangwa alisema; vijana na wazazi wenye wenye vijana wenye sifa na waliochaguliwa kujiunga wanapaswa kuchangamkia fursa hiyo ya kufika chuo mapema maana ikitokea mtu hajafika basi nafasi yake atapewa mtu mwingine.
"Tumejulishwa kuwa Chuo cha VETA cha Wilaya ya Ruangwa kitaanza kutoa mafunzo mwezi wa 6. Hivyo vijana waliochaguliwa mjiandae mapema msijepoteza nafasi hii kwani msipokuja nafasi hii watapewa vijana wa maeneo mengine" amesema Mbesigwa.
Naye mratibu wa Mafunzo Prosper Sacky (mtafiti wa soko la ajira) Kutoka ofisi ya VETA Kanda alielezea amevutiwa sana na mwitikio wa washiriki katika wilaya Ruangwa tofauti na sehemu nyingine mabazo aina hii ya mafunzo yamefanyika. ambapo kwa kawaida hunaojitokeza ni kati ya 20 hadi 30. lakini kwa wilaya Ruangwa walioomba kupata mafunzo walikuwa ni takribani 637 na walionufaika katika awamu hii ni 264.
Aliendelea kusema kutokana na mwitikio huu wa wananchi kuona thamani ya kupata elimu ili kujijengea uwezo, unemfanya atamani kurudi tena Ruangwa kwa ajili ya mafunzo mengine kadri ya uhitaji.
Pia alisisitiza umuhimu wa kujiandaa kutumia fursa zitakazotokana na ujenzi wa barabara ya Ruangwa hadi Nanganga na pia matarajio ya ujenzi wa kiwanda cha kuchakata gesi asilia kinachotarajia kujengwa Lindi kwani kutakuwa na ongezeko la mahitaji hususani vyakula,
Naye Kaimu Mkurugenzi wa VETA kanda ya kusini Bwana Elias Nzunda aliwapongeza wana Ruangwa kwa kuitikia mwito wa kupata mafunzo ili kujiongezea kipato. Aliwasisitiza kutumia chuo cha VETA cha wilaya Ruangwa ili kujikwamua kiuchumi na kwamba chuo cha VETA Ruangwa kitumike vyema kwani fani zilizopangwa kuanza zitawajenga vijana katika kuikwamua wilaya ya Ruangwa.
Pia alishukuru serikali ya Jamhuri wa Muungani wa Tanzania kupitia uongozi wa rais Samia Hasani Suluhu katika kujenga Tanzania ya wajasiliamali wenye ujuzi. Pia alimshukuru Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na (Mbunge wa Ruangwa) Mh. Kasim Majaliwa (Mb) kwa kusimamia vyema na kwadhati miundominu na maendeleo ya wana Ruangwa. Aliwasihi washiriki wa mafunzo kwenda kuwa mabalozi katika kukitangaza chuo cha VETA Ruangwa ili vijana wengi wajitokeze kujiunga na hatimae waendeleze uchumi wa wana Ruangwa.
Nao washiriki wa mafunzo walitoa risala yao ambayo wakimshukuru Rais samia Suluhu Hasa raisi wa serikali ya Muungani wa Tanzania na pia mbunge wao na waziri mkuu Mh. Kasim Majaliwa kwa kuwakumbuka na kuahidi kwambamafunzo waliyopata watayafanya kwa vitendo. Pia waliomba oungozi wa VETA ue karibu nao na kuendelea kuwalea ili hatimae waweze kufikia ndoto na malengo yao.
MWISHO
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa