Mkuu wa wilaya ya Ruangwa Mhe. Hassan Ngoma ameagiza viongozi wa vijiji na kata kuhakikisha watoto ambao hawajaripoti shule wanafanya ivyo na kuanzia tarehe 14/02/2022 mtoto ambaye hajafika shule hatua za kisheria zichukuliwe kwa yeyote anayehusika ikiwemo mtoto mwenyewe.
Amesema hayo wakati wa baraza la madiwani la kawaida la robo ya pili lililofanyika tarehe 05/02/2022 katika ukumbi wa Mkuu wa Wilaya Ruangwa mjini.
Amesema wiki ijayo atafanya msako kijiji kwa kijiji nikiwa ameambatana na mgambo ambao watakamata watoto hao watoro.
"Kama kuna mzazi anasababisha mtoto wake asifike shule kwa makusudi, acha mara moja elimu ni haki ya mtoto wako na nikibaini wapo wazazi wa hivyo tutawafikisha mahakamani" amesema Ngoma
Aliendelea kusisitiza Mkuu wa wilaya kuwa suala la uachaji shule na utoro holela umekithiri Ruangwa nitahakikisha nakomesha hili suala.
"Waheshimiwa madiwani nendeni mkatusaidie kuongea na wananchi katika maeneo yenu, watoto ambao hawajafika shule wafike shule mara moja tukimkatama mtoto ambaye hajafika shule huyo tunamfikisha mahakamani siku hiyo hiyo" amesema Ngoma
Naye Diwani wa kata ya Mandawa Mheshimiwa Lipei kwa niaba ya madiwani wote alisema suala la shule ni lazima na si hiyari na hata kama hao watoto wamewazaa wao ni lazima wawasomeshe.
"Sisi tunatekeleza ilani na mkuu wa Wilaya tutakupa ushirikiano katika kutafuta hawa watoto watoro hatuwezi kufumbia macho mambo muhimu kama hayo ya elimu" amesema Lipei.
Alisema Mheshimiwa Lipei sisi ni viongozi ila ni wazazi pia, kumuona mtoto anaacha shule kwa makusudi haivumiliki hivyo tutakusaidia kuhakikisha wanarudi shule.
Mwisho
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa