Mkuu wa Wilaya Mheshimiwa Hassan Ngoma amewataka wananchi wa Ruangwa kushirikiana na serikali kwani ndiyo inayoshughulika na changamoto ambazo wawakilishi wao wanawasemea ili kuleta maendeleo katika maeneo yao.
Amesema hayo leo 15/06/2022 wakati wa mkutano wa hadhara katika kijiji cha Mbecha, Mchenganyumba na Nanganga wakati wa ziara yake ya kikazi anayoendelea kuifanya.
Mheshimiwa Ngoma alisema serikali iliyopo madarakani inapaswa kuungwa mkono na si kuanza kuipinga na kutengeneza figisu kwa lengo la kuikwamisha.
"Kushirikiana na viongozi wetu kutaharakisha maendeleo katika maeneo yetu, mkianza kuwapinga ni kurudisha maendeleo nyuma" amesema Ngoma
Aliendelea kusisitiza huu ni wakati wa kufanya kazi na si kupiga kampeni na maneno maneno, kiongozi aliyepo madarakani hata kama hukumchagua ni wajibu kufanya naye kazi kwasababu haturudii uchaguzi wala hatuna mpango wa kufanya uchaguzi kabla ya muda wake.
Vilevile Mheshimiwa Ngoma aliwataka wananchi kujianda kwa zoezi la sensa ya watu na makazi ambalo linatarajiwa kufanyika tarehe 23/08/2022
Toeni ushirikiano kwa makarani wa sensa watakaopita katika maeneo yenu, toeni taarifa za sahihi siku hiyo.
MWISHO
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa