Uchaguzi wa Serikali za Mitaa umepangwa kufanyika Novemba 27, 2024.
Akitoa tangazo la Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa mwaka 2024 Jijini Dodoma, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mohamed Mchengerwa amesema nafasi zinazowaniwa katika uchaguzi huo ni pamoja na Wenyeviti wa Vijiji, Wajumbe wa Halmashauri ya Vijiji, Wenyeviti wa Vitongoji, Wenyeviti wa Mitaa na Wajumbe wa Kamati za Mitaa.
Amesema ukomo kwa viongozi waliopo sasa ni Oktoba 28, 2024.
Waziri Mchengerwa ameongeza kuwa fomu za wagombea wa nafasi hizo ambao ni kutoka vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu zitaanza kutolewa Novemba Mosi hadi 07, 2024 na kampeni za uchaguzi zitaanza Novemba 20 hadi 26,2024.
Kufuatia kutangazwa kwa tarehe ya kufanyika kwa uchaguzi huo wa Serikali za Mitaa, Waziri Mchengerwa amemuelekeza Mkurugenzi wa TAMISEMI kuhakikisha kuanzia Agosti 16, 2024 elimu ya upigaji kura inaanza kutolewa kwa wananchi ili waweze kufahamu namna ya kushiriki katika uchaguzi huo.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa