• Anuani zetu |
    • Maswali na Majibu |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Ruangwa District Council
Ruangwa District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Uongozi wa Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Ardhi
      • Elimu Msingi
      • Afya
      • Maji
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Fedha na Biashara
      • Elimu Sekondari
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Usafi na Mazingira
      • Kata
    • Vitengo
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Ugavi
      • Nyuki
      • Sheria
      • Uchaguzi
      • Tehama
    • Kata
      • Nandagala
      • Mbekenyera
      • Likunja
      • Mnacho
        • Nangumbu
      • Malolo
      • Nachingwea
      • Ruangwa
      • Makanjiro
      • Mbwemkuru
      • Narungombe
      • Nangumbu
      • Luchelegwa
      • Chinongwa
      • Mandawa
      • Chunyu
      • Matambarale
      • Nkowe
      • Nambilanje
      • Nanganga
      • Namichiga
      • Mandarawe
      • Chibula
      • Chienjele
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Madini
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za Kudumu
    • Ratiba
  • Mradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi ya Afya
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Videos
    • Hutuba
    • Albamu ya Picha
    • Habari
    • Tukio
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari

Tutatumia sheria kwa wazazi wasiopeleka watoto shule

Posted on: February 3rd, 2023

Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Mkoani Lindi Hassan Ngoma   amesema kuanzia February 6 2023 wataanza kufanya msako mtaa kwa mtaa, nyumba kwa nyumba kwa kutumia sheria na miongozo iliyopo  kwa wazazi wasio wapeleka Watoto shuleni msako huo ni ili kubaini watoto ambao hawajaripoti shuleni kwa wale waliofaulu kuingia kidato cha kwanza pamoja na watoto waliofika umri wa kuanza darasa la kwanza na awali. 

Ngoma ameyasema hayo leo alipokuwa anazungumza na Ruangwa fm Radio ofisini kwake wakati akibainisha  hatua zinazoendelea kuchukuliwa kwa wazazi wasiowapeleka watoto wao shuleni huku akibainisha  kuwa kwa sasa wanaendelea kufanya ziara katika kata mbali mbali za Wilaya  ambapo mpaka hivi sasa tayari wameshazungumza na wazazi na walezi katika kata 12 kati ya kata 20  ambapo matarajio  ni mnamo kufikia mpaka jumamosi ya February 4  watakuwa wamekamilisha kwa kata 8 zilizosalia.

Akizungumzia hali ya uandikishwaji wa wanafunzi kwa madarasa ya awali na la kwanza Afisa Elimu awali na Msingi halmashauri yawilaya ya  Ruangwa mwalimu George Mbesigwe amesema mpaka sasa halmashauri hiyo wamevuka lengo la maoteo ya uandikishaji wa wanafunzi ambapo mpaka sasa wameshafika asilimia 117 %

“Kwa mwaka wa masomo 2023 halimashauri  iliotea kuandikisha wanafunzi wa awali 3367 , wavulana 1664 na wasichana 1703 ambapo mpaka February 02/2023 tayari tumeandikisha wanafunzi 4087 ambao wavulana 2068 na wasichana 2019 sawa na asilimia 121%.”Amesema Mbesigwa

Hata hivyo Mbesigwe amesema zipo sababu mbali mbali zilizopelekea uandikishwaji wa wanafunzi hao kupanda ambapo ni pamoja na mabadililoko ya uandikishaji wa wanafunzi ambapo miaka ya nyuma uandikishaji huo ulikuwa ukifanyika kuanzia Desemba mpaka march na sasa unafanyika October mpaka Desemba pia uboreshwaji wa miundombinu ya mashuleni.

Kwa upande wa waalimu akiwepo Mwalimu wa darasa la awali  Neema Ngonyani Shule ya msingi Ruangwa  amesema miongoni mwa changamoto wanayokabiliana nayo walimu kwa wanafunzi wanaochelewa kuandikishwa shule ni kushindwa kuwafundisha katika mtiririko unaotakiwa huku  mwalimu wa darasa la kwanza Elizabeth Masue  akibainisha kuwa  kitendo cha wanafunzi kuchelewa kuandikishwa shule kinafanya  walimu kuwa na mlundikano wa majukumu mengi.

“ile January ninapofungua shule ninakuwa na azimio la kazi kuanzia ile wiki tunayofungulia kama ni ya kwanza  au ya pili kwa hivyo ninavyofungua natakiwa kuwafundisha wale watoto sasa mwingine anakuja wa pili mwingine wa tatu  lazima atakuwa tofauti na yule aliekuja mwezi wa kwanza hivyo inanilazimu kutafuta muda wa ziada ili kumfundisha yule aliyechelewa kufika shule ili awezekuwa  sawa na wengine vinginevyo nisipofanya hivyo nikitoa mazoezi au mitihani darasani hataweza kufanya vizuri kwa sababu vile vitu hajavisoma”amesema Mwl. Ngonyani.

Baadhi ya wazazi Wilaya ya Ruangwa wasiotaka kutaja majina yao wametaja sababu za kucheleweshwa kuripotishwa Kwa wanafunzi hadi kufika february hii ni ugumu wa Maisha hivyo kukosa baadhi ya mahitaji kama vifaa vya shule  huku Wazazi Wengi wakihamasika kupeleka watoto wao mashuleni kupitia  hamasa na elimu inayotolewa na mkuu wa wilaya kupitia ziara yake ya kata kwa kata wilayani hapa.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI HALMASHAURI YA WILAYA YA RUANGWA November 08, 2023
  • TANGAZO LA NAFASI ZA WAHUDUMU WA AFYA 872 KWA NGAZI YA JAMII HALMASHAURI YA WILAYA YA RUANGWA July 09, 2024
  • TANGAZO LA AJIRA HALMASHAURI YA WILAYA YA RUANGWA August 01, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA RUANGWA March 13, 2023
  • Ona zote

Habari mpya

  • MKURUGENZI WA RUANGWA AHIMIZA USAFI NA MAZOEZI KWA AJILI YA AFYA BORA

    May 10, 2025
  • SMAUJATA YAENDESHA ELIMU DHIDI YA UKATILI WA KIJINSIA KWA WASICHANA RUANGWA

    May 09, 2025
  • BURIANI

    May 07, 2025
  • MHE. MAJALIWA AAINISHA MAFANIKIO MAKUBWA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO RUANGWA CHINI YA UONGOZI WA RAIS SAMIA

    May 03, 2025
  • Ona zote

Video

MAENDELEO YATAKUJA KWA KULIPA USHURU, TOZO NA ADA ZA HALMASHAURI. MWANANCHI LI0A KODI KWA MAENDELEO YETU
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • Mpango wa Bajeti 2017/2018(MTEF)

Kurasa zinazofanana

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • BARAZA LA MITIHANI

Idadi ya Wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Mahali

Anuani zetu

    Ruangwa

    Anuani ya Posta: S.L.P 51

    Simu ya Mkononi: 0732932312

    simu: 0732932312

    Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera za Usiri
    • Kanusho
    • Maswali na Majibu
    • Ramani ya Eneo
    • Huduma

Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa