Baraza la waheshimiwa madiwani Wilayani Ruangwa limeitaka Halmashauri hiyo kuunda sheria ndogo zinazowabana wakulima wanaofanya kilimo cha kuhamahama.
Pia wamewataka viongozi wa dini kuendelea kutoa elimu za ndoa ili kuepusha talaka ambazo zinasababisha familia kusambaratika na watoto kukosa haki zao za msingi.
Hayo wameyasema wakati majadiliano ya kimkakati juu ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto yaliyofanyika ukumbi wa Rutesco Ruangwa mjini leo tarehe 29/2019 yaliyoendeshwa na Chama cha Wanahabari wanawake Tanzania (TAMWA).
Naye Makumu Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe Shabani kambona alikiri kuwepo kwa matendo ya ukatili na unyanyasaji kwa watoto wa kike.
Aidha alisema kumekuwa na tabia za watoto wa kike kutumia njia za uzazi wa mpango ilihali ni wanafunzi hali hii inasababisha kuongezeka kwa vitendo ngono kwa watoto.
Naye Meneja wa Ufuatiliaji na Tathimini bwana John Ambros alipata fursa ya
kuuelezea mradi mbele ya Madiwani , wakuu wa Idara na wadau wengine.
Pia alishukuru kwa ushirikiano tulioupata kutoka Halmashaur ya Wilaya ya Ruangwa kwani wameweza kutimiza malengo ya mradi huo.
Meneja Ambrose amesema mradi tuliofanya tunatamani uendele kusisitizwa huko vijijini nyie ni watu wa karibu sana na jamii mkatusaidie kusisitizi kupinga mila na desturi zenye kusababisha madhara katika jamii
Aidha Kwa ujumla wake mradi umebainisha changamoto za uwepo wa mila potofu kwa jamii zinazosababisha matendo ya kikatili kwa wanawake na watoto kama vile vipigo,ndoa za utotoni,ulawiti na ubakaji, na watoto kupelekwa kwenye jando na unyago katika umri mdogo
MWISHO
ISERT
AMBROSI
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa