Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa ndg, Frank Fabian Chonya amegawa baiskeli, fimbo za wasioona na jozi kwa watu wenye ulemavu Ruangwa na amewataka vifaa hivyo vitumike vizuri kwa watu wenye walemavu
Ndugu Chonya Amegawa vifaa hivyo tarehe 08/02/2021 katika makao makuu ya ofisi ya Halmashauri mjini Ruangwa.
"Aliendelea kusema nikikuta baiskeli hizi zinatumika na mtu asiyesitahiki nitamnyang'anya na kumpa mtu mwenye uhitaji maan huwezi kupewa wewe baiskeli alafu ukampa mtu asiyenauhitaji" amesema Chonya
Aliendelea kusema uongozi wa Halmashauri katika kusimamia mikopo hiyo haipotei itatoa wataalamu wa kumsimamia na kumsaidia kukuza biashara yake mnufaika wa mikopo.
Naye Diwani wa kata ya Nkonwe aliwataka watu wenye ulemavu kutumia vifaa hivyo katika kujiongezea kipato ili kuboresha maisha yao
Pia amewaomba kutumia fursa ya mikopo itakayotolewa ya mtu mmoja mmoja na kuitumia katika uzalishaji wa kila siku.
Naye Rehema Mitachi mnufaika wa vifaa vilivyogaiwa aliushukuru uongozi wa Halmashauri kwa kuona haja ya kuwagawia mikopo hiyo.
Aliendelea kusema anaomba mikopo hiyo itakapotolewa kila mnufaika atakaepokea pesa basi azifanyie biashara na arudishe mkopo huo ili na wanufaika wengine waweze kukopa.
Msaada wa vifaa hivyo umetolewa na Kampuni ya Sigara Tanzania imetoa baiskeli 28, magongo jozi 50 na fimbo za wasioona 100.
MWISHO
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa