Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Ruangwa Mhe Rashid Nakumbiya amebainisha upungufu wa damu ya kuhifadhi katika Halmashauri ya wilaya ya Ruangwa
Kauli hii imetoka leo tarehe 26/02/2020 wakati waheshimiwa madiwani wakichangia damu kwa hiari katika hospitali ya Wilaya iliyopo Ruangwa mjini.
Mheshimiwa Nakumbya ametoa wito kwa wananchi wa Ruangwa kujitokeza kwa wingi katika zoezi hili la uchangiaji damu kwa hiari katika hospitali ya Wilaya, vituo vya Afya zahanati na popote panapofanyika huduma hiyo
“ uhitaji wa damu katika hospitali yetu ni mkubwa wananchi jitoeni kuchangia damu na mchukulie suala hili kama suala linalomgusa kila mtu ili kumaliza tatizo hili la upungufu wa damu” Nakumbiya
Alisema Mheshimiwa Nakumbiya kwa uzito wa jambo hili waheshimiwa madiwani ambao hawajabahatika kufika na kutoa damu leo, siku ya baraza la madiwani tarehe 5-6/03/2020 watapata nafasi ya kutoa damu kwa hiari.
Vilevile Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma za Jamii, Diwani wa kata ya Nandagala Mhe Andrea Chikongwe amewataka waheshimiwa madiwani kutumia mikutano yao ya hadhara kuhamasisha wananchi kuchagia damu.
Pia Mhe Chikongwe amewataka wananchi wa Ruangwa kuwa wazalendo katika kushughulikia changamoto za Wilayani humo kwasababu changamoto hizo zinawagusa moja kwa moja
“Tusikae tukisubiri kuletewa damu kutoka nje ya Wilaya changamoto hii ni ndogo sana inaweza kumalizwa na wanaruangwa sisi wenyewe tujitokeze kwa wingi ili kuwe na damu ya kuhifadhi kwa wingi na itasidia hata mtu unapopata mgonjwa itasaidia kupata damu kwa uharaka”Chikongwe
Naye Mratibu wa damu salama wa Wilaya Alex Habron alisema zoezi la uchangiaji damu salama halina madhara yoyote kwa mchangiaji hivyo watu wajitokeze kwa wingi katika kuchangia damu
Aidha alisema zoezi liliofanyika leo limefika asilimia 50 na ni zoezi endelevu wananchi wasiogope kwani kutoa damu hakuna gharama yoyote anayoitoa mchangiaji ili kutoa damu hiyo.
“Mtu mmoja akichangia damu anakuwa amekoa maisha ya wagonjwa ambao wanauhitaji wa damu naomba wananchi wajitokeze kwa wingi zoezi halina masharti magumu na hakuna mtu atatoa damu bila kupimwa kama anasitahiki kutoa damu hiyo mjitokeze kwa wingi.
Mratibu Alex alisema zoezi hili ni endelevu na ndiyo limeanza litafika mpaka vijijini ila kwasasa wananchi wajitokeze kwa wingi katika hospitali ya Wilaya ili kufanikisha malengo ya kuwa damu kwa wingi katika wilaya ya Ruangwa.
MWISHO
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa