• Anuani zetu |
    • Maswali na Majibu |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Ruangwa District Council
Ruangwa District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Uongozi wa Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Ardhi
      • Elimu Msingi
      • Afya
      • Maji
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Fedha na Biashara
      • Elimu Sekondari
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Usafi na Mazingira
      • Kata
    • Vitengo
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Ugavi
      • Nyuki
      • Sheria
      • Uchaguzi
      • Tehama
    • Kata
      • Nandagala
      • Mbekenyera
      • Likunja
      • Mnacho
        • Nangumbu
      • Malolo
      • Nachingwea
      • Ruangwa
      • Makanjiro
      • Mbwemkuru
      • Narungombe
      • Nangumbu
      • Luchelegwa
      • Chinongwa
      • Mandawa
      • Chunyu
      • Matambarale
      • Nkowe
      • Nambilanje
      • Nanganga
      • Namichiga
      • Mandarawe
      • Chibula
      • Chienjele
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Madini
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za Kudumu
    • Ratiba
  • Mradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi ya Afya
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Videos
    • Hutuba
    • Albamu ya Picha
    • Habari
    • Tukio
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari

TUENDELEE KUMPA USHIRIKIANO RAIS WETU - MAJALIWA

Posted on: September 10th, 2023

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amewataka wananchi waendelee kumuamini Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa sababu ana dhamira na malengo makubwa ya kuendelea kuboresha maendeleo katika maeneo mbalimbali nchini yakiwemo na ya wilaya ya Ruangwa.

“Tujenge imani ya Serikali yetu, tujenge imani na Rais wetu Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kuwa anatupenda na amedhamiria kutuletea maendeleo. Hapa katika kata ya Nanganga tumejengewa shule ya sekondari iliyogharimu shilingi milioni 470, watoto wanasoma. “ 

Mheshimiwa Majaliwa ameyasema hayo leo (Jumapili, Septemba 10, 2023) wakati akizungumza na wananchi katika vijiji vya Mbecha, Nangumbu, Chimbila na Michenga akiwa katika ziara ya kukagua maendeleo wilayani Ruangwa, Lindi.

Waziri Mkuu amesema Serikali imeidhinisha fedha nyingi kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo zikiwemo shilingi bilioni 169 kujenga mradi wa maji wa Nyangao-Ruangwa ambao utanufaisha wananchi katika vijiji 34 vya Ruangwa na 12 vya Nachingwea.

Amesema kukamilika kwa mradi huo kutasaidia kupunguza tatizo la upatikanaji wa maji safi na salama kwa wananchi waishio katika vijiji hivyo pamoja na vijiji vyote ambavyo mradi huo utapita, amewaomba wananchi hao waendelee kuwa na subira na imani na Serikali yao.

Ameongeza kuwa katika kuhakikisha wilaya hiyo inakuwa na miundombinu bora ya barabara Rais Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan aliridhia kutoa kiasi cha shilingi bilioni 69 kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya Nanganga-Ruangwa kwa kiwango cha lami.

Naye, Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel amesema Serikali imefanya maboresho makubwa katika hospitali ya mkoa wa Lindi kwa kufunga mashine ya CT Scan iliyogharimu kiasi cha shilingi bilioni mbili, hivyo imewapunguzia wananchi safari ya kwenda Dar es Salaam kwa ajili ya kufuata kipimo hicho.


Amesema mbali na maboresho hayo pia, hospitali ya Kanda ya Kusini iliyoko mkoani Mtwara nayo imeanza kutoa huduma kwa wananchi. “Badala ya wananchi kwenda kufuata huduma za rufaa Muhimbili huduma hizo watazipata Mtwara. “ 

Kwa upande wao, wenyeviti wa vijiji waliishukuru Serikali kwa jitihada zake za kuboresha huduma mbalimbali za kijamii katika maeneo yao zikiwemo za afya, maji, elimu na miundombinu. “ Suala la afya tupo vizuri, tuna zahanati ya kisasa na kuhusu maji wanatapa maji safi na salama, “ alisema Mwenyekiti wa kijiji cha Mbecha Twalib Nandonde.

 

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI HALMASHAURI YA WILAYA YA RUANGWA November 08, 2023
  • TANGAZO LA NAFASI ZA WAHUDUMU WA AFYA 872 KWA NGAZI YA JAMII HALMASHAURI YA WILAYA YA RUANGWA July 09, 2024
  • TANGAZO LA AJIRA HALMASHAURI YA WILAYA YA RUANGWA August 01, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA RUANGWA March 13, 2023
  • Ona zote

Habari mpya

  • BURIANI

    May 07, 2025
  • MHE. MAJALIWA AAINISHA MAFANIKIO MAKUBWA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO RUANGWA CHINI YA UONGOZI WA RAIS SAMIA

    May 03, 2025
  • WANANCHI WA KIJIJI CHA MPARA WAFANYA USAFI KUJIANDAA NA MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU

    May 03, 2025
  • HALMASHAURI YA WILAYA YA RUANGWA YATUNUKIWA TUZO KWA KUONGOZA KATIKA VIASHIRIA VYA AFYA MKOA WA LINDI

    May 03, 2025
  • Ona zote

Video

MAENDELEO YATAKUJA KWA KULIPA USHURU, TOZO NA ADA ZA HALMASHAURI. MWANANCHI LI0A KODI KWA MAENDELEO YETU
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • Mpango wa Bajeti 2017/2018(MTEF)

Kurasa zinazofanana

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • BARAZA LA MITIHANI

Idadi ya Wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Mahali

Anuani zetu

    Ruangwa

    Anuani ya Posta: S.L.P 51

    Simu ya Mkononi: 0732932312

    simu: 0732932312

    Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera za Usiri
    • Kanusho
    • Maswali na Majibu
    • Ramani ya Eneo
    • Huduma

Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa