Afisa Mipango Ndugu Patson Massamalo sambamba na Kaimu Mkuu wa kitengo cha Miundombinu na Maendeleo ya Vijijini na Mjini Mhandisi Noel Zakaria Kitundu wakagua mradi wa ufungaji wa taa za sola vijijini leo Machi 14, 2024 katika kijiji cha Chienjele kilichopo Kata ya Chienjele Wilaya ya Ruangwa na kutoa rai kwa viongozi wa kijiji hicho kusimamia mradi ambao utawasaidia wajasiriamali wadogo wadogo katika shughuli zao za kukuza uchumi wao na kuhakikisha hazifanyiwi uhalibifu wa namna yeyote.
Mradi huo umefadhiliwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ruangwa Mheshimiwa Kassim Majaliwa ambapo kwa sasa mradi huo umetekelezwa katika kijiji cha Chienjele, Mandawa na Mbekenyera.
Kwa upande wake Mtendaji Kata wa Chienjele Ndugu Jackson Geoffrey ametoa rai kwa wananchi kutumia taa hizo vizuri katika shughuli za maendeleo hususani biashara ili kuinua uchumi wa mtu mmoja mmoja na uchumi wa Wilaya kwa ujumla.
Katika hatua nyingine, wananchi wametoa shukrani za dhati kwa Mbunge wa Jimbo la Ruangwa Mheshimiwa Kassim Majaliwa na kuahidi kutumia vyema taa hizo ambazo zitawasaidia wao katika shughuli zao za maendeleo.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa