• Anuani zetu |
    • Maswali na Majibu |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Ruangwa District Council
Ruangwa District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Uongozi wa Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Ardhi
      • Elimu Msingi
      • Afya
      • Maji
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Fedha na Biashara
      • Elimu Sekondari
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Usafi na Mazingira
      • Kata
    • Vitengo
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Ugavi
      • Nyuki
      • Sheria
      • Uchaguzi
      • Tehama
    • Kata
      • Nandagala
      • Mbekenyera
      • Likunja
      • Mnacho
        • Nangumbu
      • Malolo
      • Nachingwea
      • Ruangwa
      • Makanjiro
      • Mbwemkuru
      • Narungombe
      • Nangumbu
      • Luchelegwa
      • Chinongwa
      • Mandawa
      • Chunyu
      • Matambarale
      • Nkowe
      • Nambilanje
      • Nanganga
      • Namichiga
      • Mandarawe
      • Chibula
      • Chienjele
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Madini
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za Kudumu
    • Ratiba
  • Mradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi ya Afya
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Videos
    • Hutuba
    • Albamu ya Picha
    • Habari
    • Tukio
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari

Timu ya Soka Namungo Yapata Wadhamini

Posted on: May 25th, 2018
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema timu ya soka ya Namungo ya Wilaya ya Ruangwa imepata udhamini wa sh. milioni 150 katika msimu ujao wa ligi daraja la kwanza.


Waziri Mkuu ambaye pia ni Mbunge wa Ruangwa, ametoa kauli hiyo  wakati akizungumza na mamia ya wananchi na viongozi wa wilaya na mkoa mara baada kukagua uwanja mpya unaojengwa katika kijiji cha Dodoma, kata ya Nachingwea, wilayani Ruangwa, mkoani Lindi.


Amesema timu hiyo ambayo imepanda daraja msimu huu wa ligi, imefanikiwa kupata mdhamini mkubwa ambaye ni kampuni ya Haojue ya kutoka China inayouza pikipiki za aina ya SanLG.



“Bado tuko kwenye mazungumzo na kampuni ya Uranex, hivi sasa wako mbioni kukamilisha taratibu za udhamini, na wakikubali watakuwa wadhamini wetu namba mbili,” alisema.


Aliyataja makampuni na taasisi nyingine ambazo zimeshatoa udhamini kwa timu hiyo kuwa ni Ngureme Co. Ltd (madini), Lindi Jumbo Ltd (madini), Benki ya NMB, Halotel, CocaCola (ambao wametoa mipira 25 na jezi), Mzee Bakhresa, kampuni ya AZAM, kampuni ya Nazareth, Masoud Jaba na Gemini Exploring Ltd.


Alisema hivi sasa kocha wa timu hiyo anaendelea na usajili wa wachezaji kwa ajili ya msimu ujao, na tayari wachezaji 17 wamekwishasajiliwa, na wengine 10 bado wanaendelea kufuatiliwa.


Waziri Mkuu aliishukuru kampuni ya Haojue kwa kukubali kuidhamini timu hiyo. “Tuna uhakika kwamba wana-Namungo hawatalala njaa wakiwa kambini,” alisema.


Kwa upande wake, mshauri wa kampuni ya Haojue hapa nchini, Bw. Martin Mbwana alisema wamekubali kuwa wadhamini wakuu kwa gharama ya sh. milioni 150 kwa mwaka na udhamini wao utajumuisha jezi na viatu vya wachezaji.

(mwisho)


Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI HALMASHAURI YA WILAYA YA RUANGWA November 08, 2023
  • TANGAZO LA NAFASI ZA WAHUDUMU WA AFYA 872 KWA NGAZI YA JAMII HALMASHAURI YA WILAYA YA RUANGWA July 09, 2024
  • TANGAZO LA AJIRA HALMASHAURI YA WILAYA YA RUANGWA August 01, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA RUANGWA March 13, 2023
  • Ona zote

Habari mpya

  • MKURUGENZI WA RUANGWA AHIMIZA USAFI NA MAZOEZI KWA AJILI YA AFYA BORA

    May 10, 2025
  • SMAUJATA YAENDESHA ELIMU DHIDI YA UKATILI WA KIJINSIA KWA WASICHANA RUANGWA

    May 09, 2025
  • BURIANI

    May 07, 2025
  • MHE. MAJALIWA AAINISHA MAFANIKIO MAKUBWA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO RUANGWA CHINI YA UONGOZI WA RAIS SAMIA

    May 03, 2025
  • Ona zote

Video

MAENDELEO YATAKUJA KWA KULIPA USHURU, TOZO NA ADA ZA HALMASHAURI. MWANANCHI LI0A KODI KWA MAENDELEO YETU
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • Mpango wa Bajeti 2017/2018(MTEF)

Kurasa zinazofanana

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • BARAZA LA MITIHANI

Idadi ya Wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Mahali

Anuani zetu

    Ruangwa

    Anuani ya Posta: S.L.P 51

    Simu ya Mkononi: 0732932312

    simu: 0732932312

    Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera za Usiri
    • Kanusho
    • Maswali na Majibu
    • Ramani ya Eneo
    • Huduma

Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa