Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa, umeanza leo Jumatano, tarehe 2 Julai 2025, zoezi la malipo ya ruzuku kwa kaya 3,896 za walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kutoka Vijiji 90 vya Wilaya hiyo, zoezi hilo linatarajiwa kuendelea hadi Ijumaa, tarehe 4 Julai 2025.
Katika mpango huo, jumla ya kaya 3,302 zitapokea malipo yao kwa njia ya taslimu, ambapo kiasi cha shilingi 38,518,000 kimetengwa kwa ajili hiyo. Aidha, kaya nyingine 2,594 zitapokea ruzuku kwa njia ya kielektroniki kupitia simu au benki, na zitatumia jumla ya shilingi 75,702,000.
Hatua hiyo ni sehemu ya jitihada za Serikali kupitia TASAF katika kupunguza umasikini kwa kutoa ruzuku inayolenga kuboresha hali za maisha ya wananchi, hasa katika maeneo ya vijijini. Hata hivyo, Mamlaka husika zimeeleza kuwa maandalizi yamekamilika na zoezi linaendelea kwa utulivu.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa