Umoja wa Wakuu wa Shule za Sekondari Wilaya ya Ruangwa (TAHOSSA) leo Mei 22, 2025 umekabidhi seti tatu za jezi kwa wanafunzi watakaoshiriki mashindano ya Umoja wa Michezo kwa Shule za Sekondari Tanzania (UMISSETA), ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono maendeleo ya michezo wilayani humo.
Makabidhiano hayo yamefanyika katika Ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa yakiongozwa na Mwenyekiti wa TAHOSSA wilayani humo, Mwalimu Eugene Mtoshu, aliyemkabidhi jezi hizo Afisa Elimu Sekondari wa Wilaya ya Ruangwa, Mwalimu Ernest George Haule.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mwalimu Mtoshu alisema msaada huo ni sehemu ya juhudi za wakuu wa shule kuinua vipaji vya michezo kwa vijana na kuimarisha ushiriki wa shule za sekondari Ruangwa katika mashindano ya kimkoa na kitaifa.
Kwa upande wake, Mwl. Haule ameushukuru umoja huo kwa mchango wao, akisisitiza kuwa utasaidia kuhamasisha wanafunzi kushiriki kikamilifu mashindano hayo ya kila mwaka.
Mashindano ya UMISSETA hukutanisha wanafunzi kutoka mikoa mbalimbali nchini kwa lengo la kuibua na kuendeleza vipaji vya michezo miongoni mwa vijana.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa