Uongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Songwe, wametembelea katika wilaya za Nachingwea na Ruangwa mkoani Lindi kwa ajili ya kujifunza shughuli za uendeshaji wa maghala ya kuhifadhi mazao ya biashara korosho na ufuta sambamba na kujifunza kuhusu mfumo wa uuzaji kupitia stakabadhi mazao ghalani ambao umekua ukinufaisha kwa kukizipatia mapato Halmashauri zinazotumia mfumo huo.
Hatua hiyo inakuja kufuatia Halmashauri ya songwe kutaka kuanza kutumia mfumo wa mauzo mazao stakabadhi ghalani katika mazao ya ufuta na korosho ambazo wameanza kuzalisha na kuachana na utaratibu wa uuzaji holela ambao unawanyima mapato Halmashauri n ahata wakulima kutonufaika kutokana na uuzaji holela.
Akiwa katika ghala la lipande wilayani Ruangwa Novemba 15,2022 linalotumika kuhifadhia mazao Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Songwe Cecilia Kavishe, aliesema lengo la ziara yao ni kujifunza kuhusu mfumo wa stakabadhi ghalani kwa madiwani na wataalamu wa halamashauri ya Songwe ambapo hivi karibuni wanategemea kwenda kuanza kuutumia mfumo huo, huku Afisa kilimo wilaya ya Songwe Mfilinge Abdulkadiri akieleza kupata suluhisho la matatizo baada ya kujifunza uendeshaji wa mfumo huo na kuona utakavyosaidia kutatua changamoto za soko kwa wakulima.
“Tumewaleta madiwani na wataalam wajifunze kuhuus namna ya kuendesha ghala lakini pia kujifunza kuhusu mfumo huu wa stakabadhi ghalani” alisema mkurugenzi wa Songwe
Awali walipotembele katika ghala la Lipande wilayani Ruangwa wakapata maelekezo ya maana ya Stakabadhi Ghalani kutoka kwa meneja wa ghala hilo Asha Ramadhani, huku Afisa kilimo wa wilaya ya Ruangwa Nolasco kilumile akibainisha faida wanazopata Halmashauri ikiwa ni Pamoja na kutoza faini pale mnunuzi anaposhindwa kutoa mzigo kwa wakati ghalani baada ya kuununua.
Inakadiriwa Mapato yanayotokana na ghala katika kipindi cha msimu wa mauzo ya mazao katika ghala la lipande Ruangwa ni Zaidi ya milioni 70 kwa kila tani 1500 zinazouzwa kutoka ghala hilo ambapo fedha hizo uingia kama sehemu ya mapato ya Halmashauri.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa