Katika kuadhimisha siku ya wanawake Duniani, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Mhe. Rashidi Nakumbya, ambaye alikuwa ni mgeni rasmi katika maadhimisho hayo, amewataka wazazi kuelekeza zaidi nguvu kwa watoto wa kike kwa kuwapa elimu bora na kuwatengenezea mazingira salama ya kuishi.
Amesema hayo leo 08/03/2019 wakati wa maadhimisho ya Siku ya wanawake yaliyofanyika mjini Ruangwa katika kiwanja cha CWT.
Mheshimiwa Nakumbya amesema kumuendeleza kielimu mtoto wa kike kuna faida maana mtoto wakike anaweza kusoma mpaka elimu ya juu na bado akakumbuka kuisaidia familia yake.
Pia ametoa rai kwa wanaume kuwaruhusu wake zao kujishughulisha na shughuli za kimaendeleo kwa manufaa ya familia nzima ,wanaume tunajichelewesha kuwakataza wanawake wasifanye kazi au shughuli yoyote ya kuingiza kipato tunasahau kuwa maisha ni kusaidiana, mwanamke anapopata basi familia nzima inakuwa imepata.
Pia amewataka wanawake kutumia fursa wanazozipata kwa ufasaha na kuacha kufanya matumizi ya fedha bila mpangilo, vikoba vinawasaidia wanawake ila kuna wengine mmeanza vitumia vibaya mnakopa kurudisha inakuwa shida hembu fuateni taratibu za kukopa, kutumia na kurudisha kama mnavyoelekezwa
Vile vile amewataka wanawake kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi za uongozi kwani kiongozi mwanamke mara nyingi huwa ni muadilifu
Naye Diwani wa viti maalumu Paulina ametoa rai kwa wanaume kuwaachia wanawake uhuru wa kujishugulisha katika kutafuta kipato ili kusaidiana majukumu ya ndani.
Naye mwanamke aliyepata zawadi ya kuwa mwanamke shupavu kwa ujasiriamali Anusyata Cosmas ameishukuru Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa kwa mikopo na elimu wanayowapatia wajasiriamali katika kikundi chao.
Bi Anusyat amewataka wanawake kutokata tamaa kwani ujasiriamali unalipa kama zilivyo kazi nyingine na kupitia ujasiriamali huo ameweza kujenga nyumba na kusomesha mtoto wake shule ya binafsi.
MWISHO
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa