Kupitia mafunzo ya utawala bora, Mwezeshaji Mwalimu Uzima Milele Justine ameshauri serikali za vijiji kufanya kazi kwa uwazi na kutoa taarifa kwa wananchi kwa wakati.
Ametoa ushauri huo wakati wa mafunzo ya utawala bora yanayofanyika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Wilaya leo 16/06/2022 Ruangwa mjini.
Alisema ndg Uzima, serikali ya kijiji ikitaka kufikisha malengo yake basi ifuate kanuni za uwazi na usawa na kuzingatia kutoa taarifa kwa wananchi kwa wakati.
"Si sahihi kuwapa wananchi taarifa viporo hivyo wenyeviti wa vijiji wahakikishe taarifa wanayotoa kwa wananchi ni ya muda husika".
Alisema kutoa taarifa viporo kwa wananchi husababisha sintofahamu katika maeneo mengi kwasababu wananchi wana uelewa na vikao vinavyotakiwa kufanyika.
Aidha aliwaomba watumie lugha nyepesi wakati wa uwasilishaji wa taarifa zao kwa wananchi, hii itapelekea uelewa wa kutosha kwa wananchi.
Alisema lengo la mikutano ni kutoa taarifa kwa wananchi hivyo wanapaswa kuelewa kile kinachowasilishwa ili kuondoa sintofahamu katika wananchi katika mambo wanayowasilishiwa
Mafunzo haya yanaratibiwa na Jukwaa la Elimu ya Uraia Tanzania (CETA) yanayohusisha wenyeviti wa vijiji, watendaji wa Vijiji na Wenyeviti wa Kamati za Kudumu za Vijiji, mafunzo haya yanamlengo wa kuwafikia viongozi wote Wa serikali ya vijiji 90 vya Ruangwa.
MWISHO
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa