Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Mheshimiwa Joseph Mkirikiti ametoa shukurani kwa Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kwa msaada wa vifaa vya ujenzi lililoutoa katika shule mpya ya Sekondari ya Kassim Majaliwa iliyopo Ruangwa Mjini.
Shirika la Nyumba la Taifa limetoa msaada wa bati 300 na mifuko ya saruji 300 katika shule mpya ya Kassim Majaliwa ikiwa ni kwa lengo la kuanza ujenzi wa Maabara shuleni hapo.
Mheshimiwa Mkirikiti aliliomba shirika hilo lisichoke kutoa msaada kwani shule hiyo bado ni changa na ina mahitaji mengi ya miundo mbinu ambayo hayajakamilika kujengwa pia alilitoa hofu kwa kusema kuwa vifaa vilivyotolewa vitatumika kama inavyotakiwa.
“Tunataka shule hii iwe ni shule ya mfano katika Mkoa wa Lindi hivyo vifaa vilivyotolewa tutavitumia vizuri katika kujenga miundombinu yenye hadhi inayohitajika ili kuifanya shule hii kuwa imara na ya kudumu”, alisema Mh,Mkirikiti.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa