• Anuani zetu |
    • Maswali na Majibu |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Ruangwa District Council
Ruangwa District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Uongozi wa Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Ardhi
      • Elimu Msingi
      • Afya
      • Maji
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Fedha na Biashara
      • Elimu Sekondari
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Usafi na Mazingira
      • Kata
    • Vitengo
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Ugavi
      • Nyuki
      • Sheria
      • Uchaguzi
      • Tehama
    • Kata
      • Nandagala
      • Mbekenyera
      • Likunja
      • Mnacho
        • Nangumbu
      • Malolo
      • Nachingwea
      • Ruangwa
      • Makanjiro
      • Mbwemkuru
      • Narungombe
      • Nangumbu
      • Luchelegwa
      • Chinongwa
      • Mandawa
      • Chunyu
      • Matambarale
      • Nkowe
      • Nambilanje
      • Nanganga
      • Namichiga
      • Mandarawe
      • Chibula
      • Chienjele
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Madini
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za Kudumu
    • Ratiba
  • Mradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi ya Afya
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Videos
    • Hutuba
    • Albamu ya Picha
    • Habari
    • Tukio
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari

SHILINGI MILIONI 920 KUJENGA SHULE MBILI ZA SEKONDARI RUANGWA

Posted on: February 20th, 2024

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ameridhia kutoa sh milioni 920 kwa ajili ya ujenzi wa shule mbili za Sekondari ikiwemo za Namakuku na Namichinga, Wilayani Ruangwa ikiwa ni muendelezo wake wa koboresha sekta ya elimu nchini


Amesema ujenzi wa Shule hiyo utasaidia wanafunzi katika maeneo hayo kutotembea umbali mrefu kufuata shule “Nawapongeza sana wakazi wa Namakuku kwa uamuzi wenu wa kutoa eneo kwa ajili ya ujenzi wa shule, huku ni kumuunga mkono Rais Dkt. Samia”


Amesema hayo Jumanne (Februari 20, 2024) wakati alipokagua maendeleo ya ujenzi wa Zahanati Namakuku pamoja na Taa za barabarani kwenye kata ya Chienjele, Ruangwa Mkoani Lindi.


Akizungumza kuhusu ujenzi wa Zahanati hiyo, Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa zahanati ambayo ni jitihada za Wananchi pamoja na Ofisi ya Mbunge ina vyumba vyote muhimu “Mmejenga jengo kubwa lenye vyumba vingi vyenye hadhi ya kituo cha Afya, mganga mkuu wa wilaya amekagua na amegundua linafaa kuwa kituo cha afya kidogo”


Amesema kuwa katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia, Wilaya ya Ruangwa imepata mabadiliko makubwa katika sekta zote za maendeleo “Niliamua kuwaita viongozi wa Chama cha Mapinduzi ili wasikie mambo makubwa yaliyofanywa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan hapa Ruangwa “lazima tumshukuru Mheshimiwa Rais Dkt. Samia ametufanyia mambo makubwa sana”


Wakizungumza katika mikutano hiyo Diwani wa Kata ya Chienjele Rashidi Nnunduma na Diwani wa Viti Maalum wa Kata hiyo Dalini Mbira, wameishukuru Serikali ya Awamu ya sita inayoomgozwa na Rais Dkt . Samia kwa miradi ya meendeleo kwenye sekta za maji, kilimo, elimu, afya na uwezeshaji wananchi kiuchumi.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI HALMASHAURI YA WILAYA YA RUANGWA November 08, 2023
  • TANGAZO LA NAFASI ZA WAHUDUMU WA AFYA 872 KWA NGAZI YA JAMII HALMASHAURI YA WILAYA YA RUANGWA July 09, 2024
  • TANGAZO LA AJIRA HALMASHAURI YA WILAYA YA RUANGWA August 01, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA RUANGWA March 13, 2023
  • Ona zote

Habari mpya

  • MKURUGENZI WA RUANGWA AHIMIZA USAFI NA MAZOEZI KWA AJILI YA AFYA BORA

    May 10, 2025
  • SMAUJATA YAENDESHA ELIMU DHIDI YA UKATILI WA KIJINSIA KWA WASICHANA RUANGWA

    May 09, 2025
  • BURIANI

    May 07, 2025
  • MHE. MAJALIWA AAINISHA MAFANIKIO MAKUBWA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO RUANGWA CHINI YA UONGOZI WA RAIS SAMIA

    May 03, 2025
  • Ona zote

Video

MAENDELEO YATAKUJA KWA KULIPA USHURU, TOZO NA ADA ZA HALMASHAURI. MWANANCHI LI0A KODI KWA MAENDELEO YETU
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • Mpango wa Bajeti 2017/2018(MTEF)

Kurasa zinazofanana

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • BARAZA LA MITIHANI

Idadi ya Wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Mahali

Anuani zetu

    Ruangwa

    Anuani ya Posta: S.L.P 51

    Simu ya Mkononi: 0732932312

    simu: 0732932312

    Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera za Usiri
    • Kanusho
    • Maswali na Majibu
    • Ramani ya Eneo
    • Huduma

Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa