• Anuani zetu |
    • Maswali na Majibu |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Ruangwa District Council
Ruangwa District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Uongozi wa Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Ardhi
      • Elimu Msingi
      • Afya
      • Maji
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Fedha na Biashara
      • Elimu Sekondari
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Usafi na Mazingira
      • Kata
    • Vitengo
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Ugavi
      • Nyuki
      • Sheria
      • Uchaguzi
      • Tehama
    • Kata
      • Nandagala
      • Mbekenyera
      • Likunja
      • Mnacho
        • Nangumbu
      • Malolo
      • Nachingwea
      • Ruangwa
      • Makanjiro
      • Mbwemkuru
      • Narungombe
      • Nangumbu
      • Luchelegwa
      • Chinongwa
      • Mandawa
      • Chunyu
      • Matambarale
      • Nkowe
      • Nambilanje
      • Nanganga
      • Namichiga
      • Mandarawe
      • Chibula
      • Chienjele
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Madini
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za Kudumu
    • Ratiba
  • Mradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi ya Afya
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Videos
    • Hutuba
    • Albamu ya Picha
    • Habari
    • Tukio
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari

Shilingi bil. 222 zimelipwa kwa wakulima wa korosho- Majaliwa

Posted on: December 30th, 2018

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema jumla ya shilingi bilioni 222 zimelipwa na Serikali kwa wakulima wa zao la korosho na kuwataka wakulima wawe na subira.

Amesema wakulima walioanza kulipwa ni wale wenye kilo zisizozidi kilo 1,500 na wale wenye kilo zaidi ya 1,500 na kuendelea Serikali inaendelea na uhakiki kisha watalipwa.

”Fedha zipo, hakuna mkulima ambaye atapoteza haki yake wote watalipwa. Tunaendelea na uhakiki kwa wale wenye korosho nyingi ili kubaini kama hawajanunua kangomba.”

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumapili, Desemba 30, 2018) alipozungumza na wananchi wa kijiji cha Nandagala ‘A’ baada ya kufungua ofisi ya CCM kata ya Nandagala.

Amesema baadhi ya watu wamekutwa na kilo zaidi ya 1,500 na wameshindwa kuonesha mashamba yao ya mikorosho, hali inayodhihirisha kwamba amenunua kupitia kangomba.

Waziri Mkuu amesema baadhi ya waliokutwa na korosho nyingi ni vijana wadogo ambao hawana hata uwezo kifedha hivyo Serikali itahakikisha inawakamata watu wanaowatuma.

Amesema lengo la Serikali inayoongizwa na Rais Dkt. John Magufuli ni kuhakikisha wakulima wananufaika na kilimo chao, hivyo biashara ya kangomba lazima lidhibitiwe.

Waziri Mkuu ambaye leo ameanza ziara yake kwa kikazi wilayani Ruangwa, Mkoani Lindi amesema zoezi la ulipaji kwa wakulima wa korosho linaendelea, wakulima wawe na subira.

Serikali iliamua kununua korosho zote za mwaka huu baada ya kubaini wafanyabiashara wamepanga kuwadhulumu wakulima kwa kupanga kununua kwa bei ndogo.

Wakati huo huo, Waziri Mkuu ametembelea eneo la ujenzi wa shule ya sekondari ya kata ya Matambalale wilayani Ruangwa ambapo amewataka wahakikishe ujenzi unakamilika.

Amewataka wananchi wa kata hiyo kushirikiana na kuhakikisha wanachangia nguvu kazi katika ujenzi wa vyumba vya madarasa ili mwakani wanafunzi waanze kusoma.

”Tunataka tuondoe dhiki ya watoto wetu kutembea umbali mrefu hadi Namichiga kutafuta elimu, tunataka watoto wetu wote wasome katika maeneo yaliyo karibu na makazi yao.”

Amesema wanafunzi zaidi ya 200 wamefaulu na hawana pa kwenda hivyo ni lazima ujenzi wa shule zote za sekondari za Matambalale, Chibura na Luchelegwa ukamilike.

Waziri Mkuu amesema hadi Januari 10, 2019 shule hizo zote lazima ujenzi wake ukamilike ili wanafunzi waanze kusoma, hivyo viongozi washirikiane na wananchi kukamilisha ujenzi.

Mwisho



Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI HALMASHAURI YA WILAYA YA RUANGWA November 08, 2023
  • TANGAZO LA NAFASI ZA WAHUDUMU WA AFYA 872 KWA NGAZI YA JAMII HALMASHAURI YA WILAYA YA RUANGWA July 09, 2024
  • TANGAZO LA AJIRA HALMASHAURI YA WILAYA YA RUANGWA August 01, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA RUANGWA March 13, 2023
  • Ona zote

Habari mpya

  • MKURUGENZI WA RUANGWA AHIMIZA USAFI NA MAZOEZI KWA AJILI YA AFYA BORA

    May 10, 2025
  • SMAUJATA YAENDESHA ELIMU DHIDI YA UKATILI WA KIJINSIA KWA WASICHANA RUANGWA

    May 09, 2025
  • BURIANI

    May 07, 2025
  • MHE. MAJALIWA AAINISHA MAFANIKIO MAKUBWA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO RUANGWA CHINI YA UONGOZI WA RAIS SAMIA

    May 03, 2025
  • Ona zote

Video

MAENDELEO YATAKUJA KWA KULIPA USHURU, TOZO NA ADA ZA HALMASHAURI. MWANANCHI LI0A KODI KWA MAENDELEO YETU
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • Mpango wa Bajeti 2017/2018(MTEF)

Kurasa zinazofanana

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • BARAZA LA MITIHANI

Idadi ya Wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Mahali

Anuani zetu

    Ruangwa

    Anuani ya Posta: S.L.P 51

    Simu ya Mkononi: 0732932312

    simu: 0732932312

    Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera za Usiri
    • Kanusho
    • Maswali na Majibu
    • Ramani ya Eneo
    • Huduma

Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa