Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe. Kassim Majaliwa amesema kuwa, Serikali imetoa tsh.billioni 1.4 kwa ajili ya uboreshaji wa vituo vya afya katika wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi.
Ameyasema hayo wakati alipotembelea kata ya mandawa kwa ajili ya kukagua mradi wa uboreshaji wa kituo cha afya cha kata hiyo wakati wa Ziara yake ya kikazi Wilayani humo.
“Serikali imeamua kuimarisha sekta ya afya kwa kujenga na kuboresha vituo vya afya li kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za afya na kwa karibu na makazi yao.” Amesema Waziri Mkuu
Mhe. Waziri Mkuu amesema kati ya fedha hizo sh. Million 400 kwa ajili ya kituo cha afya Mandawa, sh. Milioni 500 kituo cha afya Mbekenyera na sh. Milioni 500 kituo cha afya Nkowe.
Amesema uboreshaji huo unahusisha ujenzi huo chumba cha upasuaji, maabara, chumba cha kujifungulia kina mama, wodi ya mama na mtoto na wodi ya wanawake na wanaume na chumba cha kuhifadhia maiti.
Aidha, Mhe. Majaliwa amewataka wananchi hao waendelee kuiunga mkono serikali yao, ambayo imedhamiria kuwatumikiaili waweze kupata maendeleo.
Pia Waziri Mkuu amekabidhi gari la kutolea huduma za afya vijijini. Gari hilo linauwezo wakutoa huduma za afya kama Zahanati kwani lina vitanda vitatu vya kulaza wagonjwa na litakuwa linatembea na manesi na daktari kwa ajili ya kutoa huduma.
“Huduma ya afya inazidi kuimarika kuanzia sasa kutakuwa na gari linaloenda katika vijiji vilivyombali na zahanati kwa ajili ya kuwapatia wananchi huduma umsiliogope kwani ni kama zahanati zetu” amesema Waziri Mkuu.
Katika hatua nyingine, Mhe. Waziri Mkuu ameshiriki katika zoezi la ufyatuaji wa matofali kwa ajili ya ujenzi wa shule ya sekondari ya Kata ya Matambalale ambayo itakuwa inahudumia Vijiji visivyopungua vinne.
Amesema kata hiyo yenye vijiji vinne ilikuwa haina shule ya sekondari,hivyo kusababisha wanafunzi kutembea umbali wa kilomita tano kwenda kusoma kwenye shule za kata nyingine.
“Serikali inataka kumlinda mtoto wa kike apate elimu bila usumbufu wowote awali watoto wa kike wa kata ya matambalale walikuwa wanatembea umbali mrefu au kupanga mitaani hali ambayo inahatarisha usalama wao, baada ya kukamilika ujenzi wa shule hii watoto wakike watasoma katika mazingira mazuri” amesema Waziri Mkuu
Naye mwanakijiji wa kata wa Matambarale bi Zuhura Idi amesema wanaushukuru uongozi wa Halmashauri kwa kuona jinsi watoto wao wanavyopata shida na kuamua kuwasaidia katika kuhakikisha inapatikana shule ya sekondari katika kata hiyo.
“Wananchi wa kata ya Matambarale tutashirikiana na uongozi wa halmashauri kwa hali na mali katika kufanikisha zoezi hili la ujenzi wa shule kukamilika kwani watoto wetu hasa wa kike wanapata elimu katika mazingira magumu”amesema bi Zuhura.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa