Wananchi Wilayani Ruangwa Mkoani Lindi wameipongeza serikali ya awamu tano kwa maamuzi yake ya kuwaondolea tatizo la upatikanaji wa huduma za afya za uhakika hasa maeneo ya vijijini kwa kuanzisha ujenzi wa vituo vya afya na ukurabati wa majengo ya zamani vitakavyo gharimu shilingi bilioni 1.4 Wilayani humo.
Katika Ziara ya kikazi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi Godfrey Zambi wananchi hao wameonyesha furaha yao wakati wakiungana katika ukaguzi wa baadhi ya ujenzi wa vituo hivyo unaoendelea.
Moja ya kituo ambacho Mkuu wa Mkoa wa huyo alipata fulsa ya kuongea na baadhi ya wakazi hao ni pale alipofika katika kata ya mbekenyela na kujionea ujenzi wa kituo cha mbekenyela,ambapo baadhi ya wakazi hao wakaonyesha dalili ya kuondokana na adha ambayo wamekuwa wakiipata ikiwemo kusafiri umbali kufuata huduma za afya pamoja na kukosekana kwa vifaa na vyumba maaluma vya kujifungulia hali waliyoeleza kuwa kukamilika kwa vituo hivyo kunaweza kutatua changamoto hizo.
“Tulikuwa tukipata taabu sana hasa wakati wa usiku lakini pia mara kadha tumeshindwa kupata huduma stahiki katika kitu chetu hasa pale tunapokosa maeneo muhimu kwa mama wajawazito hii ni kukoseka na kwa vyumba mbadala kwa wazazI” Alisema Subira Mkaminje Mkazi wa Mbekenyela.
“Sasa mama mjamzito akiandikiwa upasuaji inambidi atoke kijijini hata siku 3 kabla ya tarehe ili awahi mjini kupata huduma ya upasuaji lakini vituo hivi vikikimalika suala hili litasahaulika ashukuriwe Rais wetu mpendwa”Aliongeza bi Subira.
Ujenzi huo wa vituo vya afya ni utaratibu wa serikali katika kusambaza huduma muhimu na bora kwa wananchi wake ambapo tayari Wilaya ya Ruangwa inatarajia kukamilisha ujenzi wa vituo vya afya vitatu.
Naye bwana Hamisi Mbina alisema tunasababu nyingi za kumshukuru na kumpongeza Rais wetu John Pombe Magufuli kwani amefanya sasa tunapata huduma nzuri tunapokwenda katika zahanati zetu au vituo vya Afya.
“Nitakuwa mchoyo wa fadhira kama sitomshukuru Mbunge wa jimbo letu kwa kutupigania wananchi wake na kuhakikisha tunapata huduma bora kwasasa kila kituo cha afya katika Wilaya ya Ruangwa kina gari za kubebea wagonjwa zote hizi ni jitihada na Mbunge wetu”amesema Hamisi.
Mkuu wa Mkoa wa Lindi alifanya ziara yake kujionea shughuli za ujenzi unaondelea katika vituo vya mbekenyela,mandawa na Nkowe na kuzitaka kamati kusimamia kikamilifu ujenzi huo kwakuwa serikali imedhamiria kutekeleza miradi itakayowanufaisha wananchi wake.
“Hizi fedha serikali imezitoa ili kufanikisha utekelezaji wa ujenzi wa vituo vya afya ambavyo vikikamilika tutawaondolea wananchi changamoto walizokuwa wanazipata hapo awali,sasa Mkurugenzi na Watendaji wote nawaagiza msikae maofisini tu simamieni matumizi ya fedha hizi pamoja na kufanya ukaguzi wa mara kwa mara katika maeneo yote ya ujenzi unaoendelea. Amesema mkuu wa mkoa huyo.
Wilaya ya Ruangwa ni moja kati ya wilaya sita zilizipo mkoani Lindi,kufuatia upanuzi na ukarabati wa vituo hivyo tayari mkoa unaendelea na ujenzi wa vituo 13 vinavyogharimu kiasi cha shillingi billon 6.2 na kwa mujibu wa maagizo ya serikali vinatakiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi October 30 mwaka huu.
MWISHO.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa