Shirika la Sport Development Aids (SDA) lenye makao yake nchini Finland, limeendesha mafunzo ya maadili na huduma ya kwanza kwa kundi la ngariba na kungwi wa Wilaya ya Ruangwa, Aprili 15, 2025, katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri.
Mafunzo hayo yamelenga kuwawezesha washiriki kuelewa masuala ya msingi ya maadili katika malezi ya kijamii pamoja na namna ya kutoa huduma ya kwanza kwa watu waliopata changamoto za kiafya kama kuvunjika, kujeruhiwa au kupoteza fahamu.
Aidha, Mkurugenzi wa SDA Mkoa wa Lindi, ndugu Lamso Lucas Albano, amewaongoza wageni kutoka Finland kutoa mafunzo hayo ambayo yamelenga kuelimisha washiriki juu ya umuhimu wa maadili katika malezi ya kijamii na namna ya kutoa huduma ya kwanza
“Tumeona kuna umuhimu mkubwa wa kuwafikia watu wa makundi haya kwa sababu wana nafasi ya moja kwa moja katika malezi ya watoto na vijana, hivyo ni muhimu wawe na uelewa wa maadili na huduma ya kwanza.” Amesema Albano.
Naye mmoja wa ngaliba waliopata mafunzo hayo, Mzee Said Abdalla, amesema: “Mafunzo haya yametufungua macho, sasa tunaelewa vizuri namna ya kushughulikia majeruhi kabla ya kufika hospitali, sambamba na kujitathmini kwenye maadili tunayoyasimamia.”
SDA ni shirika linalotoa elimu ya maadili kwa jamii na kusaidia vifaa vya michezo kwa vijana, likilenga kuchochea maendeleo chanya kupitia ushirikiano na wadau mbalimbali ndani na nje ya Tanzania.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa