Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa kupiti Idara ya Afya itaendesha zoezi la utoaji wa dawa za tiba na kinga kwa magonjwa ya Minyoo tumbo na Kichocho kwa watoto walioko shule za msingi zilizopo katika Halmashauri hiyo.
Akitoa taarifa mbele ya kamati ya Afya ya Msingi ya Wilaya katika kikoa kilichofanyika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ,Mratibu wa Magonjwa yasiyopewa kipaumbele Paschal Thobias Lutubija amewaambia wajumbe kuwa zoezi la utoaji wa dawa hizo litafanyika kuanzia tarehe 2-3 mwezi Mei mwaka huu ,hivyo amewataka wajumbe kutoa hamasa kwa jamii ili kuweza kufanikisha zoezi hili.
Kwa upande wake Kamanda wa Taasisi ya Kupambana ns Kuzuia Rushwa Wilaya ya Ruangwa Bwana James Mwakambonja ameitaka Idara ya Afya ambayo itaratibu zoezi hilo kufanya kazi kwa uadilifu ili kazi iliyokusudia ifanyike na kuonyesha thamani ya fedha ambayo itafanana na kazi iliyofanyika.
Pia amewaonya watendaji ambao wamekuwa na tabia za ujanjaujanja wa kufanya matumizi ya fedha nje ya shughuli zilizokusudiwa na mradi husika, amesema taasisi yake haitasita kuchukua hatua kwa watendaji wa Idara watakao kwenda kinyume katika matumizi ya fedha hizo.
Naye Daktari Bakari Nampeha aliwaomba wazazi na wanafunzi wanaotarajiwa kupata dawa hizi wazione dawa hizi ni sawa na zile zinazotolewa kila siku katika vituo vya kutolea huduma za afya kwamba hazina tofauti kabisa na hazina madhara kwa binadamu.
Katibu Tawala wa wilaya ya Ruangwa Twaha Mpembenwe ambaye alikuwa mwenyekiti wa kikao akimwakilisha Mkuu wa Wilaya alisisitiza utoaji wa taarifa katika ofisi yake ili aweze kufanya tathimini juu ya zoezi hili
Pia amewata kuwa waadilifu katika utendaji kazi wao na kuwakumbusha kuwa wanafunzi ndiyo taifa la kesho na ili mwanafunzi aweze kusoma vyema anapaswa awe na afya bora hakikisheni zoezi hili linamfikia kila mlengwa.
MWISHO
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa