Washiriki wa mafunzo ya ufugaji kuku na samaki wamepata mafunzi ya namna ya kufunga na kuandaa bwawa la samaki.
Mafunzo hayo wameyapata leo tarehe 19/05/2022 katika chuo cha Veta nandagala Ruangwa washiriki wa mafunzo hayo wametoka katika kata tisa zilizopo ruangwa ambazo ni Kata ya Nandagala, Likunja, Nkowe, Chienjere, Mnacho, Nanganga, Ruangwa Nachingwea na Malolo.
Mkufunzi Emanueli Madinda amewahamasisha washiriki wa mafunzo hayo kuanzisha mabwawa ya samaki katika maeneo yako kwani ufugaji samaki si kazi wala mgumu kama watu wanavyoambiana
Eliendelea kusema kufuga samaki kunaitaji muda na kufuata taratibu za ufugaji ukifanya hivyo ufugaji samaki utakuwa mwepesi na utazoeleka kama ufugaji kuku.
Alisema Veta wamefanya jambo kubwa sana kuratibu zoezi hili la utoaji elimu ya ufugaji kuku na samaki na endapo washiriki wakizingatia mafunzo haya ni lazima awe mfugaji bora wa samaki.
Naye mshiriki wa mafunzo Mwalimu Lusia Chitanda amesema alikuwa anatamani kujishughulisha na suala ufugaji samaki muda mrefu ila hakuwa na elimu ila anashukuru veta kwa kuwaletea mafunzo haya.
Alisema akitoka hapa anaenda kuwa mfugaji samaki, maana samaki ni chanzo kizuri cha mapato hapa ruangwa kwasababu kwasasa samaki ruangwa kilo ni shilingi elfu kumi na niwaombe washiriki wenzangu tukitoka hapa tuanze kufuga samaki najua tumezoea kufuga kuku ila sasa tufuge samaki wanalipa.
Aliendelea kusema baada ya kupata taarifa ya mafunzo haya alifurahishwa sana na ndiyo maana ameshiriki Ila aliwaomba uongozi wa veta kuendelea kutoa mafunzo ya ufugaji samaki ili wazidi kuwa wafugaji bora wa samaki ruangwa
MWISHO
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa