Kituo cha Redio Jamii Ruangwa FM kimetoa tuzo kwa wanawake waliotoa mchango mkubwa katika maendeleo ya jamii, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani ngazi ya Wilaya ya Ruangwa yaliyofanyika leo Machi 5, 2025, katika viwanja vya Shule ya Msingi Likangara.
Katika hafla hiyo, Bi. Sada Chonya ametunukiwa Tuzo ya Mwanamke Mpambanaji kutokana na kujitoa kwake katika shughuli zote za maendeleo ndani ya jamii. Bi. Fatuma Mkokoya naye ametunukiwa Tuzo ya Mwanamke Mjasiriamali Bora na mfano wa kuigwa kwa wanawake na jamii kwa ujumla.
Aidha, Timu Galauka imetunukiwa Tuzo ya Kikundi Bora cha Wanawake Wazalendo kwa kuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha maendeleo ndani na nje ya Wilaya ya Ruangwa.
Tuzo hizo zimetolewa kama sehemu ya kuthamini juhudi za wanawake katika kuleta maendeleo, huku Redio Ruangwa FM ikiahidi kuendelea kuhamasisha ushiriki wa wanawake katika sekta mbalimbali kwa ustawi wa jamii.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa