Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mheshimiwa Godfrey Zambi amewataka Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa kufuatilia kwa ukaribu utendaji kazi wa Wataalamu wa Halmashauri hiyo.
Waheshimiwa madiwani mnatakiwa kiwasimamia wataalamu wa Halmashauri hii bila kuangalia ukaribu wala urafiki uliopo baina yenu na inapobainika mtu anamakosa sheria na taratibu zifuate kama inavyotakiwa.
Mkuu wa Mkoa amesema hayo wakati wa Mkutano maalumu wa Baraza la Madiwani wa kupitia hoja maalumu za ukaguzi mwaka wa 2016/2017 katika ukumbi wa Rutesco mjini Ruangwa.
Ambapo Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa imepata hati inayoridhisha, hati hii hutolewa wakati wa Mkaguzi ameridhia kuwa hakuna dosari zozote katika hesabu na taarifa za fedha zimeandaliwa kwa mujibu wa mfumo na viwango vya uandaaji taarifa za fedha zinavyokubalika kitaifa na kimataifa
“Hili ni duka ni lenu na wataalamu ni wauzaji wenu na mjue wao wanakuja na kuondoka mara kwa mara ili nyie mnakuwepo kwa muda mrefu hivyo ni wajibu kujua mauzo ya duka hilo kwa ukaribu”amesema Zambi
Pia aliwataka kufuata Sheria na taratibu zinazowekwa na kufuata sheria hizo si hiari kwa menejimenti wala madiwani na maagizo ya serikali yakija ni wajibu wao kuyatekeleza kama yanavyoagizwa” amesema Mheshimiwa Zambi.
“Shirikianeni katika utendaji kazi mtafanikiwa kwani hakuna kitu kizuri kama ushirikiano katika kutekeleza majukumu mtafika mbali mkifanya kazi kwa pamoja na mtaifikisha mbali zaidi kwa upande wa maendeleo Wilaya hii”amesema Zambi.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Andrea Chezue alimhakikishia Mkuu wa mkoa kufunga hoja zilizokuwa zimebaki kutokana na mipango iliyowekwa na Menejitimenti.
Amesema Mkurugenzi Chezue kati ya hoja 57 za nyuma, 43 zimejibiwa kikamilifu na kufugwa na hoja 14 zilizobaki zipo katika hatua za utekelezaji na hoja za ukaguzi kwa mwaka 2016/2017 zipo 22 ambazo zinaendelea kujibiwa.
“Ushauri na mapendekezo ya wakaguzi yanazingatiwa na inatarajiwa katika kipindi cha ukaguzi wa hesabu wa za Halmashauri zinazoishia juni 2018 zitahakikiwa”amesema Chezue
Aidha Mkurugenzi Mtendaji Andrea Chezue alitumia nafasi hiyo kutangaza mchezo wa kirafiki baina ya Simba na Namungo fc utakaofanyika katika uwanja mpya wa michezo Ruangwa mjini agosti 11, 2018.
MWISHO
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa