Mkuu wa Mkoa wa Lindi Godfery Zambi amewataka wakurungenzi wa Halmashauri ya Ruangwa, Liwale, Kilwa na Nachingwea kuhakikisha Zahanati zilizopo ndani ya Wilaya hizo hazifungwi kutokana na upungufu utakaojitokeza wa watumishi waliokutwa na tatizo la vyeti feki.Mh Mkuu wa Mkoa Zambi alisema wakurungenzi watendaji wa Halmashauri hizo wajitahidi kuhamisha wauuguzi watakaokuwa wengi katika eneo moja wapelekwe katika zile zahanati ambazo zinautaji zaidi ya watumishi.
Aliyasema hayo wakati akihutubia katika sherehe za siku ya wafanyakazi dunia iliyofanyika katika Wilaya ya Ruangwa kwenye uwanja wa shule ya msingi likangara ambapo inafanyika kwa mwaka mara moja mwezi wa 5 tarehe 1.Kauli hiyo imetokana na agizo alilolitoa Rais wa Jamhuri ya Muungano John Pombe Magufuli la watumishi waliokutwa na vyeti feki waache kazi mara moja laasivyo watachukuliwa hatua za kisheria.
Aidha alisema Serikali imejipanga kupambana na watumishi wazembe na wanaofanya kazi kwa mazoea kwani uongozi wa awamu hii haupo katika kulea watu wasiotaka kubadilika.Pia aliwataka walimu wa shule za msingi na sekondari waache kunung’unika kuhusu ya maslahi yao kwani manunguniko yanaweza wasababisha washindwe kufanyakazi ipasavyo na kusababisha matokea mabaya ya mitihani ya taifa.
“Serikali inajitahidi kutatua matatizo yanaowakabili hivyo ni wakati wa walimu huko mashuleni kufanya kazi kwa bidii na kubadilisha matokea ya darasa la saba na kidato cha nne kwa mwaka huu”alisema.Mkuu wa Mkoa alitumia nafasi hiyo kuwakaribisha wadau mbalimbali katika shughuli za mwenge ambazo katika mkoa wa Lindi mwenge utapokelewa tarehe 21 na wilaya ya Ruangwa tarehe 23 na 24 mwezi wa tano.
Wakati huo huo Mratibu wa Tucta mkoa wa Lindi Fatma .s. Chaunga aliomba serikali kuweza kupunguza kiwango cha kodi kwa wafanyakazi ipungue kutokana asilimia 9 mpaka 7 kwani bado hiyo asilimia 9 nikubwa kutokana na mshahara wa watumishi wengi.Pia aliomba serikali kuangalia uchumi wa viwanda uweze kuzingatia ajira kwa wazawa kwanza kwasababu kunawatu wengi wanaelimu ya kutosha kufanya kazi katika viwanda
hivyo.Hata hivyo Bi Fatma aliipongeza serikali kwa juhudi zake za elimu bure, hali hii imesababisha wazazi wengi kupata nafasi ya kupeleka watoto wao shule kwasababu hamna gharama ya ada wanayokutanayo na imesaidia kupunguza watoto wazururaji huko vijijini na mjini.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa