Mkuu wa Mkoa Mhe Godfrey Zambi amewataka viongozi wa dini kutokupokea watu wasiowafahamu katika nyumba za ibada kwa ajili ya kutunza amani ya Nchi yetu.
Mhe,Zambi alisema kumekuwa na vitendo vya mauaji vinavyoendelea nchi vinavyoharibu hali ya amani na wanaofanya hayo inasadikika wanatumia nyumba za ibada kama nguzo ya kuficha uovu wanaoufanya.
Mkuu wa Mkoa aliyasema haya wakati wa ziara yake ya siku mbili ya kikazi aliyoifanya katika Wilaya ya Ruangwa ukiwa ni muendelezo wa ziara alizozifanya katika Wilaya zote zilizopo katika Mkoa wa Lindi.
Mhe Zambi aliwataka viongozi wa dini kutumia nyumba za ibada kuwaelimisha waumini wao kutunza amani ya nchi hii kwani amani iliyopo sasa imetoka mbali hivyo ni muhimu kuitunza.
Mhe, Mkuu wa mkoa aliwataka Madiwani kusimamia katika kata zao na kufahamu kila mgeni anaeingia hapo analengo gani ili kuepusha vitendo vya mauaji vinavyotokea sehemu nyingine.
“Katika kufankisha hili naomba viongozi wa dini mikutano yote ya dini inayofanyika katika kata, vijiji, na vitongoji viongozi wenu waweze kufahamu” alisema Zambi.
Alisema Mkuu wa Mkoa bila kuangalia tofauti zetu za kidini na siasa tushirikiane katika kuleta maendeleo ya Nchi hii, amani ikitunzwa maendeleo yatakuja kwa uharaka.
Aidha Mhe, Zambi alipiga marufuku shughuli za unyago kufanyika wakati wa kipindi cha masomo na atakaekaidi hilo achukuliwe hatua za kisheria kwani kinachofanyika ni kinyume na utaratibu.
Wakati huo huo Mkuu wa Wilaya Joseph Mkirikiti aliahidi kufuatilia na kutekeleza maagizo yote aliyoyatoa Mkuu wa Mkoa wakati wa Ziara hiyo na ataanza na la kuhakikisha kila mkazi wa Ruangwa anachoo cha kudumu nyumbani kwake.
Pia aliwataka vijana wa mbekenyera walioomba kujiunga na jeshi la akiba kwasasa waanzishe kikundi cha kukimbia ikiwa ni moja ya njia ya kuweza kufanya mazoezi ya pumzi.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa