Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe, Godfrey Zambi amewataka Wakuu wa Wilaya ya Ruangwa na Nachingwea kumaliza mgogoro wa aridhi kati ya kijiji cha Nagurugai na Mbute
Ametoa agizo hilo tarehe 17/12/2020 kwenye mkutano na wananchi wa kijiji cha Nagurugai alipofanya ziara ya kikazi Wilaya ya Ruangwa.
Mhe Zambi aliwataka wakuu wa wilaya za Ruangwa na Nachingwea kutatua suala hilo kabla ya mwisho wa mwezi disemba, 2020. Alihimiza wakutane na kukubaliana kumaliza mgogoro unaoendelea katika wilaya hizo mbili.
“Ikifika mwezi wa kwanza nitarudi kuona mmemaliza jambo hilo" katika kufanikisha hilo Zambi aliwata maafisa aridhi wa Wilaya zote mbili wasienda likizo mpaka jambo hili liishe.
Pia aliwataka wana Ruangwa kufanya kazi kwa bidii na kuacha uvivu wa kukaa vijiweni ili wabadili hali zao za kimaisha katika maeneo yao.
“Kilimo nacho ni kazi watu acheni kudharau shughuli za kilimo, ukifanya kazi kwa kuipenda na kuithamini utafanikiwa msitegeme kuajiriwa tu muwe wajasiliamali pia”amesema Zambi
Vile vile amewataka wananchi wa Ruangwa kuacha mara moja kutumia nafaka katika upikaji wa pombe kwani kutumia nafaka kwa pombe ni uharibifu wa chakula.
Aliendelea kusema Serikali imekataza kutumia nafaka katika shuguli za upikaji pombe hivyo ni wajibu wa wananchi kutii agizo la serikali kuacha kuharibu chakula kwa matumizi ya pombe.
Aidha aliwataka Viongozi wa Serikali za Vjiji kuhakikisha na kusimamia ujenzi wa vyoo vyenye staha katika vijiji vyao. Alitaka kuhakikisha choo cha kudumu na mtu asipotii agizo la anachukukiwa hatua ikiwa ni pamoja na kutozwa faini ya shilingi elf hamsini.
Akizungumzia elimu alisisitizia kuwa kila Serikali kijiji ihakikishe kila mtoto aliyefaulu kidato cha kwanza anahidhuria shule zinapofunguliwa
“Ikitokea mzazi amekaidi kupelekea mtoto shule basi achukuliwe hatua za kisheria sitaki ikifika mwezi wa kwanza kukawa na watoto wazururaji mtaani asiyetii hatua za kisheria zichukuliwe” aliagiza Zambia
MWISHO
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa