Waziri Mkuu na Mbunge wa Jimbo la Ruangwa Mhe. Kassim Majaliwa leo Julai 3, 2024 amezungumza na wakazi wa kijiji cha Mmawa kilichopo katika kata ya Nandagala, Ruangwa Mkoani Lindi.
Akizungumza na Wakazi hao Mheshimiwa Majaliwa amesema Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amedhamiria kuendelea kufikisha huduma za jamii ikiwemo Afya, maji, Umeme na Elimu katika maeneo yote nchini.
“Kwa mfano katika Wilaya ya Ruangwa na Nachingwea tuna mradi mkubwa wa maji wa shilingi bilioni 119, kwa mradi huu maeneo mengi hapa yatapata huduma ya maji. Rais Dkt. Samia pia aliamua kununua mitambo ya kuchimbia visima vya maji lengo ni kuongeza kiwango cha upatikanaji wa maji kwenye maeneo yetu.”
Aidha, Mheshimiwa Majaliwa amewataka maafisa kilimo nchini kuweka mpango wa kuwahamasisha na kuwasimamia vijana kuingia katika kilimo cha bustani kwenye maeneo ya mabonde yanayofaa kwa kilimo.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa