Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa inayoongozwa na Mheshimiwa Hassan Ngoma yafuturisha makundi mbalimbali ya wananchi ambapo Mkuu wa Wilaya amewataka viongozi kujumuika kwa pamoja na wananchi katika mambo mbalimbali ya kijamii.
" Hatua ya Viongozi wa Halmashauri kuungana na wananchi kujumuika katika kugawa chakula hii inadhihirisha wazi kwamba hakuna tofauti baina ya viongozi na wananchi" Amesema Ngoma
Ameyasema hayo leo April 05, 2024 katika zoezi la kugawa iftari lililofanyika katika eneo la Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa iliyoandaliwa na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya.
Aidha Ngoma amewashukuru wote waliohudhuria hafla hiyo kwa kukubali kuacha majukumu yao na kuamua kuungana na viongozi wa Halmashauri ili kufanikisha zoezi hilo la iftari.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Mheshimiwa Andrew Chikongwe amemshukuru Mhe. Ngoma kwa kuwaunganisha watu wa Ruangwa na kupata chakula kwa pamoja kwani si jambo rahisi bali ni kipawa.
Katika hatua nyingine viongozi wa dini ambao wameudhuria hafla hiyo wametoa wito kwa wananchi kuendelea kupendana na kushirikiana katika mambo mbalimbali ya kijamii halikadhalika kujiweka karibu na Mwenyezi Mungu kwa kufanya yale yanayompendeza.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa