.Watendaji wa kata na vijiji wilaya ya ruangwa wamehofia Hali kuwepo Kwa njaa katika miezi miwili ijayo katika kata zao na vijiji Kwa kutolima mazao ya chakula na kulima tu mazao ya biashara huku wananchi wakitegemea kununua vyakula.
Watendajiwamebainisha hayo katika kikao Kazi kilichofanyika Leo tarehe17 October 22 katika ukumbi wa mkuu wa wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi kilichojumuisha wakuu wa idara kamati ya ulinzi na usalamavakiwemo mkuu wa wilaya ya nachingwea ambae amekaimu ukuu wa wilaya ya ruangwa Ndg. Hashmu Komba.
Wakizungumza Kwa nyakati tofauti tofauti Watendaji hao akiwemo Mtendaji wa kata ya nanganga Said Ngitu amesema Uzalishaji wa mazao ya chakula Hali sio nzuri kwani wao wanalima mazao ya biashara hivyo wakifeli hapo kwenye chakula hufeli zaidi huku akibainisha Hali ya hewa huchangia wakulima kutolima mazao ya chakula.
Naye Mohamed Mapanje Mtendaji kata Nkowe amebainisha Chakula Kwa ujumla wake Hali ni tete hivyo baada ya miezi miwili inaweza Kua mbaya kutokana na Hali ya uzalishaji wa mazao ya biashara lakini pia Hali ya hewa iliyopo na mfumoko wa bei wa vyakula madukani.
Awali akitoa taarifa ya Hali ya chakula Kwa niaba ya DYCO afisa kilimo Mawazo Mkolasi amebainisha kuwa zaidi ya 90% wakazi wa Ruangwa ni wakulima hivyo Hali ya chakula hadi kufika December ni toshelezi lakini Kwa mwezi kuanzia January itabidi kununua kutoka maeneo mengine.Hata hivyo DC Komba ameomba kuazimia kufanyika kikao cha maafisa kilimo kata na vijiji ili kuandaa mikakati ya kitu gani kifanyike kulingana na maeneo ya Ruangwa na Hali ya hewa ilivyo"Naomba DAYCO katika hicho kikao kinachofuata uje na ramani ya kilimo ya wilaya ili kujua Hali ya hewa,aridhi ya eneo husika na mje na mikakati nini kifanyikeā€¯Amesema Komba
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa