Wazazi Kutoka katika kata ya Chinongwe Wilayani Ruangwa Mkoani Lindi watakiwa kuwapa nafasi watoto wao wa kike kusoma ili kupata elimu itakayowawezesha kulisaidia Taifa kukuza uchumi na kuboresha maisha yao ikiwa ni pamoja na kuzifikia ndoto zao.
Hayo yamesemwa katika viwanja vya shule ya msingi Chinongwe kata ya Chinongwe WIlayani Ruangwa na Mwalimu Mkuu wa shule ya Sekondari Chinongwe Mwalimu Propronius Kashaija Rutazamba alipokua akizungumza katika Tamasha liloandaliwa la kumwelimisha mtoto wa kike kujitambua.
Aidha amesema mtoto wa kike akielimika ni sawa na kuielimisha jamii hivyo amehimiza wazazi kuwapa nafasi watoto wa kike wasome ili waweze kulisaidia Taifa katika kuongeza kasi ya maendeleo, huku akieleza pamoja na kuwa watalisaidia Taifa lakini hata wazazi wenyewe watanufaika na mafanikio hayo na kusema kuwa ni sehemu ya matunda watakayoyafurahia.
"Binti anapopata elimu ni tofauti kidogo na mtoto wa kiume, sisi wa kiume tukishapata elimu tukishatoka kwa mfano mm nimeshatoka inamaana mimi na familia yangu hao wazazi labda nitawarushia fedha kidogo lakini motto wa kike ndie anaetegemewa hasa katika familia” Alisema Mwalimu Propronius.
Katika hatua hiyo nae Mwalimu Zaudia Juma manzi wa shule ya msingi Likunja aliefika katika Tamasha hilo kama shuhuda wa kuelezea safari yake ya mafanikio, amewataka wanafunzi kutokukatamaa kwani hata yeye alipitia majaribu na misukosuko katika wakati wake wa masomo lakini aliidhibiti na kusimamia kukamilika kwa ndoto zake na mpka sasa amefanikiwa kupata kazi ya ualimu na sasa anafurahia maisha kw kukamilisha ndoto zake.
“Kwahiyo jamani watoto wa kike tubadilike na tuipende shule ili tufikie sehemu nzuri tunazotamani kufika kwa mujibu wa ndoto zetu” Alisema Afisa Elimu kata ya Chinongwe Mwalimu Abdallah Omari Njarimbo anaelezea kufanikiwa kwa kongamo hilo huku akieleza jumla ya wasichana 951 kutoka shule za msingi Juhudi, Chinongwe, Litama na Likwachu wamepatiwa elimu hiyo na kusema kuwa anamini kutatokea mabadiliko makubwa katika kata hiyo.
Wakati huo huo wanafunzi walioshiriki kongamano hilo lililolenga kumuelimisha mototo wa kike kujikomboa Amina Rashidi Bakari wa shule ya msingi Juhudi na Martha Athumani wa shule ya msingi Chinongwe, wanaelezwa juu ya manufaa waliyoyapata kwenye tamasha hilo kuwa ni pamoja na kuhamisika juu ya kupenda elimu lakini kubwa kukamilisha kwa ndoto zao hasa kutoa mfano walioupata kwa mgeni mwalikwa na hivyo kuahidi kusoma kwa bidii ili kuyafikia malengo yao.
Hatua hii ya kongamano la kumuelimisha mtoto wa kike apate elimu ya kujitambua inakuja katika Kata hiyi ikiwa siku za hivi karibuni kuonekana ufaulu wa mtoto wa kike kushuka na kusababisha kuwa na matokeo mabaya hivyo viongozi wa elimu kata chinongwe kuona haja ya kutoa elimu na hamasa ili kuwatia moyo wanafunzi hao waweze kuongeza juhudi katika masomo yao.
Mwisho
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa