Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Mohamed Muhidini amekabidhi kuku kwa vikundi vya ufugaji viwili vya Ruangwa mjini.
Amekabidhi kuku hao tarehe 19/02/2021 kwa wanavikundi katika ofisi kuu ya Halmashauri
Alisema kaimu Mkurugenzi Halmashauri imekopesha milioni kumi na tatu na elf kumi kupitia mfuko wa maendeleo ya wanawake, vijana na walemavu kwa vikundi viwili vya ufugaji kuku.
Vile vile alisema ndugu Muhidini Halmashauri Imekopesha vikundi vya wanawake viwili ambavyo kila kimoja kimepata milioni sita laki tano na elf tano kwa mwaka wa fedha 2020/ 2021 na kutakiwa kurejesha mkopo wote kwa mwaka mmoja na vikundi hivi vyote vinapatikana mjini ruangwa.
Fedha hizi ni asilimia 10 ya mapato ya ndani yanayotengwa kutokana na vyanzo vya mapato ya ndani vya Halmashauri.
Mwisho
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa