Timu ya Namungo Fc inayoshiriki ligi daraja la kwanzaTanzania Bara msimu wa 2018/19 yenye maskani yake Wilayani Ruangwa Mkoani Lindi imepata mapokezi makubwa ilipowasili hivi leo baada ya kufuzu kuingia ligi kuu kwa kuwa na jumla ya point 43 kati kundi lake B ambapo kwa mujibu wa matokeo hayo hakuna timu yeyote ambayo inaweza kuifikia pamoja na kuwa timu hizo zimebakiza michezo miwili kwa kila moja
Namungo wamepokelewa kishujaa baada ya kuwasili hivi leo Wilayani Ruangwa wakitokea mkoani Mororogoro walipocheza mchezo dhidi ya Mawenzi Market ambao uliwapata ushindi wa magoli mawili kwa moja na kuwahakikishia kuingia ligi kuu msimu ujao.
Aidha viongozi na wadau wa soka kutoka Wilayani humo na Mkoani lindi kwa ujumla walijumuika katika kuilaki kwa kuwapongeza wachezaji wa timu hiyo huku wananchi wakisisimama kando ya barabara kuwalaki wachezaji na wadau waliokuwa katika msafara wa mapokezi Hayo.
Hamisi Mgunya ambaye yeye ni Nahodha na mchezaji mhasisisi wa Timu hiyo tokea ikiwa ligi daraja la tatu, ameelezea furaha yake kwa timu hiyo kufikia ligi kuu na kusema kuwa haikua kazi rahisi lakini kutokana na ushirikiano waliouonyesha wana Ruangwa na Mkoa wa Lindi sasa imewezekana na kuwaomba mashabiki wa soka wazidi kutoa mchango wa kuishabikia timu hiyo ili izidi kufanya vizuri inapoelekea ligi kuu msimu 2019/2020
“Nawashukuru sana wana Ruangwa ambao wametusapoti tokea kuanza kwa msimu mpaka tunapofanikiwa kwenda ligi kuu,mimi kama mchezaji nimejitahidi kupambana katika nafasi yangu tokea ligi daraja la tatu na sasa najisikia faraja sana kuona tumefanikiwa kwenda ligi kuu.”Alisema Mgunya.
Mashabiki na wadau wa soka pia wameelezea kufurahishwa kupanda kwa timu hiyo na kusema kuwa ni kufunguka kwa fursa wilayani humo ambapo zinaleta maendeleo katika sekta mbali mbali ikiwamo ya kukua kwa uchumi.
“Jambo hili ni jambo kubwa na jambo la historia kuwahi kuandikwa katika historia ya mkoa wa lindi kwahivyo ni fahari sana kwetu wana Ruangwa tuendele kuwa wazalendo kwa kuishangili timu yetu" amesema Mwenyekiti wa Halmashauri ya Ruangwa Rashidi Nakumbya.
Amesema mheshimiwa Nakumbya najua watu mnatimu zenu kubwa mnazozipenda ila kwasasa tuhamishie mapenzi na nguvu zote kwa timu yetu Namungo kwani inahitaji msaada mkubwa Ile iweze kusonga mbele tuanze kuchangia timu yetu tuanze kuipenda timu yetu Namungo
Namungo kupata point 43 na kutangaza ubingwa unatokana na kuwa mbele kwa point nane zaidi ya wanaowafuata katika kundi lake ambao ni mbeya kwanza walio na jumla ya point 35, na hivyo hata namungo akipoteza michezo miwili iliobaki bado hakuna anaeweza kufikia point hizo katika kundi lake.
MWISHO
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa