• Anuani zetu |
    • Maswali na Majibu |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Ruangwa District Council
Ruangwa District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Uongozi wa Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Ardhi
      • Elimu Msingi
      • Afya
      • Maji
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Fedha na Biashara
      • Elimu Sekondari
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Usafi na Mazingira
      • Kata
    • Vitengo
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Ugavi
      • Nyuki
      • Sheria
      • Uchaguzi
      • Tehama
    • Kata
      • Nandagala
      • Mbekenyera
      • Likunja
      • Mnacho
        • Nangumbu
      • Malolo
      • Nachingwea
      • Ruangwa
      • Makanjiro
      • Mbwemkuru
      • Narungombe
      • Nangumbu
      • Luchelegwa
      • Chinongwa
      • Mandawa
      • Chunyu
      • Matambarale
      • Nkowe
      • Nambilanje
      • Nanganga
      • Namichiga
      • Mandarawe
      • Chibula
      • Chienjele
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Madini
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za Kudumu
    • Ratiba
  • Mradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi ya Afya
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Videos
    • Hutuba
    • Albamu ya Picha
    • Habari
    • Tukio
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari

Namungo FC kupambana na Simba ya jijini DSM

Posted on: August 10th, 2018

Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa kesho (Jumamosi, Agosti, 11, 2018) inatarajia kuzindua uwanja wake wa michezo, ambapo timu ya wilaya hiyo Namungo FC inayoshiriki ligi daraja la kwanza itapambana na bingwa wa ligi kuu 2018/2019 Simba SC ya jiji Dar es Salaam.


Timu hiyo ya Namungo FC ambayo inamilikiwa na wachimbaji wa madini ya dhahabu katika eneo la Namungo wilayani Ruangwa ilianza 2009 kama sehemu ya mazoezi kwa wachimbaji hao mara wanapotoka kazini, imeupa heshima mkoa wa Lindi kwa kuwa ndiyo pekee inayoshiriki ligi daraja la kwanza.


Akizungumza wakati wa ukaguzi wa uwanja huo leo (Ijumaa, Agosti, 10, 2018) Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema mbali na timu ya Simba pia timu hiyo inatarajia kucheza na timu za Yanga , Azam za jijini Dar es Salaam na Dodoma FC ya jijini Dodoma.


Uwanja wa mpira wa miguu wa wilaya Ruangwa unaoitwa Majaliwa Stadium umejengwa katika kitongoji cha Mtichi kata ya Nachingwea na ndio utakaokuwa unatumiwa na timu ya Namungo FC kuchezea mechi za nyumbani.  


 “Lazima tuisapoti timu yetu ya Namungo FC icheze daraja la kwanza kwa mafanikio makubwa, hivyo ni vema tukashirikiana kuhakikisha timu hiyo inafanikiwa ili ndoto ya kucheza ligi kuu itimie.”


Kadhalika Waziri Mkuu amesema ni muhimu kwa timu ya Namungo FC kucheza na timu kama za Simba, Yanga, Azam na Dodoma FC kwa sababu zinasaidia katika kuimarisha viwango vya wachezaji na kuwaondolea uoga wa kupambana na timu nyingine.


Kiingilio katika mechi ya Namungo FC na Simba SC ni sh. 3000. Tayari timu ya Simba imeshawasili wilayani Ruangwa leo (Ijumaa, Agosti, 10, 2018), saa 11.01 jioni kwa ajili ya mechi yake na timu ya Namungo.

(mwisho)

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI HALMASHAURI YA WILAYA YA RUANGWA November 08, 2023
  • TANGAZO LA NAFASI ZA WAHUDUMU WA AFYA 872 KWA NGAZI YA JAMII HALMASHAURI YA WILAYA YA RUANGWA July 09, 2024
  • TANGAZO LA AJIRA HALMASHAURI YA WILAYA YA RUANGWA August 01, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA RUANGWA March 13, 2023
  • Ona zote

Habari mpya

  • MKURUGENZI WA RUANGWA AHIMIZA USAFI NA MAZOEZI KWA AJILI YA AFYA BORA

    May 10, 2025
  • SMAUJATA YAENDESHA ELIMU DHIDI YA UKATILI WA KIJINSIA KWA WASICHANA RUANGWA

    May 09, 2025
  • BURIANI

    May 07, 2025
  • MHE. MAJALIWA AAINISHA MAFANIKIO MAKUBWA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO RUANGWA CHINI YA UONGOZI WA RAIS SAMIA

    May 03, 2025
  • Ona zote

Video

MAENDELEO YATAKUJA KWA KULIPA USHURU, TOZO NA ADA ZA HALMASHAURI. MWANANCHI LI0A KODI KWA MAENDELEO YETU
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • Mpango wa Bajeti 2017/2018(MTEF)

Kurasa zinazofanana

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • BARAZA LA MITIHANI

Idadi ya Wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Mahali

Anuani zetu

    Ruangwa

    Anuani ya Posta: S.L.P 51

    Simu ya Mkononi: 0732932312

    simu: 0732932312

    Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera za Usiri
    • Kanusho
    • Maswali na Majibu
    • Ramani ya Eneo
    • Huduma

Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa