Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba, Maendeleo na Makazi Mhe. Geophrey Mizengo Pinda ametoa wito kwa viongozi kutoa elimu ya ardhi kwa wananchi kuhusu matumizi bora na endelevu ya ardhi waliyonayo.
Ameyasema hayo leo Machi 22, 2024 katika Kikao cha wadau kujadili utekelezaji wa mradi wa uboreshaji usalama wa milki za ardhi (LTIP) kilichofanyika katika ukumbi wa Ruangwa Pride Hotel wilayani Ruangwa.
Aidha Mhe. Pinda amesema kuwa vijiji vyote 90 vilivyopo Wilaya ya Ruangwa vinaenda kupitiwa na mradi wa uboreshaji usalama wa milki za ardhi (TLIP) na wananchi watapatiwa hati miliki za ardhi.
Mradi wa uboreshaji usalama wa milki za ardhi una lengo la kuimarisha Wizara kwa kuongeza na kuboresha vitendea kazi kama vile kujenga Ofisi za ardhi Mkoa na Wilaya.
Katika hatua nyingine Kamati ya matumizi bora ya ardhi ya kijiji cha Chikundi kilichopo Kata ya Mandawa wameiomba serikali kuwashika mkono katika kuhakikisha mradi unatekelezwa ipasavyo na uwe mradi endelevu katika Wilaya ya Ruangwa.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa