Naibu waziri wa Nishati Mhe, Subira Mgalu amemtaka Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa kumchukulia hatua za kisheria mkandarasi anaesambaza umeme wa REA awamu ya tatu katika wilaya ya Ruangwa endapo kama atashindwa kutimiza maagizo aliyotoa.
Naibu Waziri emeyasema hayo wakati wa halfa ya uwashaji umeme katika vijiji vitatu ambavyo ni Kijiji cha Chimbila B, Kijiji cha Mtakuja na Kijiji cha Nandaga ambapo vyote vipo ndani ya Wilaya ya Ruangwa.
"Hatuwezi kurudi nyuma na hatuwezi kubadili makubaliano yetu ya kuwa ifikapo julai 31 miradi yote ya REA 3 inatakiwa iwe imekamiliaka hivyo wakandarasi timize wajibu wenu"
“Napenda niwaambie nyie wakandarasi Serikali haijawahi kushindwa jambo hivyo hatutoshidwa kuvunja mkataba na mkadarasi kama hatotimiza wajibu wake fanyeni kazi mmebakiza muda mchache mkabidhi kazi hiyo.” amesema Mhe Mgalu.
Mhe. Mgalu amemuagiza mkandarasi huyo anaesambaza umeme wa REA kuongeza idadi ya magege ili kuongeza ufanisi na ufanyaji kazi kwa wakati na kupeleka vifaa kwa wingi katika vituo vyao vya kazi.
Vilevile amemtaka kuweka utaratibu wa kutoa taarifa kwa Mkuu wa Wilaya kila wiki kuhusiana na ufanyaji kazi wake na kuhakikisha kila wiki vijiji vitatu vinawashwa umeme kama ambavyo walivyokubaliana na serikali.
Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Mhe. Hashim Mgandilwa alisema kuwa mkandarasi amekuwa na hali ya kusuasua na kusababisha huduma ya umeme kuchelewa kupatikana kwa wananchi.
"Mhe. Naibu waziri kutokana na kasi hii anayoenda nayo mkandarasi, ni dhahiri kuwa tumempa kazi nyingi, hivyo ningeomba apunguzewe vijiji, katika mkoa wa Lindi, ni Wilaya Ruangwa peeke ndio yenye vijiji vingi vipatavyo 45 vilivyoingia katika mpango huu wa REA 3.” Alisema Mhe. Mgandilwa
Baadhi ya wananchi waliohudhurilia uzinduzi huwo walitoa malalamiko wa Naibu Waziri Kuwa wameshafuata taratibu zote za uingizwaji wa umeme ila mpaka sasa hawajafanikiwa kupata kufikiwa na umeme kwa kisingizio kuwa nguzo chache. Wamemuomba Naibu Waziri kumsimamia ili apeleke nguzo za kutosha ili waweze kupata huduma ya Umeme.
Sambamba na uwashaji umeme Naibu Waziri, amekabidhi jenereta kwa mganga mfawidhi wa kituo cha Afya Nkowe kwa niaba ya Mbunge wa jimbo la Ruangwa Mhe Kassim Majaliwa (Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania) ikiwa kama chanzo mbadala cha umeme kituoni hapo ambayo ni ahadi aliyoitoa Waziri Mkuu alipofanya Ziara ya kikazi Wilayani Hapo.
MWISHO
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa