Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Mhe. Andrew Chikongwe leo tarehe 13, Mei 2024 ameongoza kikao cha WADC cha robo ya tatu kwa mwaka wa fedha 2023/2024 katika Kijiji cha Nandagala B eneo la stendi ya mabasi.
"Tupo kwenye mapambano dhidi ya umasikini na silaha yetu kubwa ni elimu, mwalimu ameshasoma na anatumia elimu yake kuendesha maisha yake, kwahiyo wewe mzazi ambae unamwacha mtoto wako au muda mwingine unadiriki kabisa kumwambia mwanao asiende shule haumkomoi mwalimu bali unajikomoa wewe na mwanao"
Aidha Mhe. Chikongwe amewataka viongozi kuhakikisha wanafunzi wote wapo shuleni na endapo mwanafunzi yeyote hatokuwepo shuleni hatua kali zichukuliwe dhidi yake na wazazi wake.
Katika hatua nyingine, Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Nandagala amshukuru Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Mhe. Andrew Chikongwe kwa kumsaidia kuweza kupata miche 100 ya mipera na milimao kutoka Chuo kikuu cha kilimo Sokoine.
"Tunataka kufanya mapinduzi makubwa katika sekta ya kilimo, kwani wananchi wakiwa na chakuka cha kutosha hata suala la wanafunzi kula shuleni litawezekana na itakuwa chachu ya kupunguza utoro kwa wanafunzi hao" Amesema Chikongwe.
Pia, Mhe. Chikongwe amewataka Maafisa ugani kuhakikisha wanawapa mbinu za kisasa na kitaalam wakulima ili waweze kufanya kilimo chenye tija na kuachana na mazoea.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa