Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Mhe. Andrew Chikongwe akagua kiwanda cha kukamua mafuta ya alizeti kinachoendeshwa na kikundi cha Wanawake Mpitilila katika kijiji cha Nandagala Wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi.
Katika hatua hiyo ya ukaguzi wa kiwanda hicho Mhe. Andrew Chikongwe amewapongeza wanawake hao kwa kujituma, kufanya kazi kwa bidii na kwa ubunifu mkubwa na jitihada zao za kuongeza ubora wa bidhaa ya mafuta ya alizeti na karanga.
Kiwanda kinasimamiwa na kikundi cha wanawake Mpitilila ambao wamekuwa miongoni mwa wanufaika wa mkopo wa Halmashauri wa asilimia 10 unaotolewa na Serikali kwa lengo la kuwasaidia wanawake, vijana na walemavu, ambapo wao kama kikundi walipatiwa mkopo wa Milioni 30.
"Hatukufanya makosa kuhidhinisha mkopo kwa kikundi hiki kwani mpaka sasa kama kikundi wamefanya marejesho zaidi ya malengo kwa mwaka na kazi mnazozifanya ni nzuri na bidhaa zenu ni za uhakika" amesema Chikongwe.
Kikundi cha wanawake Mpitilila kimeanzishwa mwaka 2023 kikiwa na wanakikundi wanawake sita ambao walianza na kukamua mafuta ya alizeti pekee katika kiwanda hicho lakini mpaka sasa wameongeza kwa kukamua mafuta ya karanga na wana matarajio ya kuanza kutengeneza mafuta ya nazi.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa