• Anuani zetu |
    • Maswali na Majibu |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Ruangwa District Council
Ruangwa District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Uongozi wa Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Ardhi
      • Elimu Msingi
      • Afya
      • Maji
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Fedha na Biashara
      • Elimu Sekondari
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Usafi na Mazingira
      • Kata
    • Vitengo
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Ugavi
      • Nyuki
      • Sheria
      • Uchaguzi
      • Tehama
    • Kata
      • Nandagala
      • Mbekenyera
      • Likunja
      • Mnacho
        • Nangumbu
      • Malolo
      • Nachingwea
      • Ruangwa
      • Makanjiro
      • Mbwemkuru
      • Narungombe
      • Nangumbu
      • Luchelegwa
      • Chinongwa
      • Mandawa
      • Chunyu
      • Matambarale
      • Nkowe
      • Nambilanje
      • Nanganga
      • Namichiga
      • Mandarawe
      • Chibula
      • Chienjele
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Madini
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za Kudumu
    • Ratiba
  • Mradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi ya Afya
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Videos
    • Hutuba
    • Albamu ya Picha
    • Habari
    • Tukio
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari

MWENGE WA UHURU WAZINDUA MRADI WA MAJI MPARA WENYE THAMANI YA TSH MILIONI 325

Posted on: May 28th, 2025

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2025, Ndugu Ismail Ali Ussi, ameizindua rasmi mradi wa maji safi na salama katika Kijiji cha Mpara Kata ya Likunja wenye thamani ya Shilingi Milioni 325, uzinduzi huo umefanyika leo tarehe 28 Mei 2025 mbele ya wananchi, viongozi wa kijiji na wataalam wa Sekta ya maji.


Mradi huo unajumuisha uchimbaji wa visima vitano pamoja na ujenzi wa miundombinu rahisi ya maji katika vijiji vya Mmawa, Njawale, Mtawilile, Mpara na Namkatila, umeghalimu shilingi 325,000,000.00 ukiwa ni mkombozi mkubwa kwa wakazi waliokuwa wanatembea umbali mrefu kufuata huduma hiyo muhimu.

Akizungumza wakati wa kuzindua mradi huo, Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru, Comrade Ismail Ussi, amesema kuwa upatikanaji wa maji safi ni haki ya msingi kwa kila Mtanzania, na kwamba serikali itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali kuhakikisha huduma hiyo inafika maeneo yote ya vijijini.


“Mradi huu ni ushahidi wa dhamira ya serikali katika kuhakikisha wananchi wa maeneo ya vijijini hawabaki nyuma kwenye maendeleo. Maji ni uhai, na kupatikana kwake kwa urahisi ni hatua kubwa kuelekea ustawi wa jamii,” amesema Comrade Ussi.


Mwenge wa Uhuru 2025 unaendelea na ziara yake mkoani Lindi kwa lengo la kukagua, kuzindua na kuweka mawe ya msingi katika miradi ya maendeleo, huku ukiendelea kuhimiza ushiriki wa wananchi katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu kwa njia ya amani na utulivu.

Kwa ujumla, uzinduzi huo umepongezwa na wananchi wa kijiji cha Mpara na maeneo jirani, waliomshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kusogeza huduma za msingi karibu na wananchi kupitia miradi ya maendeleo inayoendeshwa kwa ushirikiano na wadau mbalimbali.


Kaulimbiu ya Mbio za Mwenge wa Uhuru 2025 inasema: “Jitokeze Kushiriki Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 kwa Amani na Utulivu.”

Matangazo

  • NAFASI ZA KUJITOLEA HALMSHAURI YA WILAYA YA RUANGWA February 13, 2026
  • FOMU YA USAJILI WA WAANDAAJI WA MAUDHUI MTANDAONI February 02, 2026
  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA RUANGWA March 13, 2023
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI April 25, 2023
  • Ona zote

Habari mpya

  • NGUVU YA HAZINA YA MADINI INAYOBADILI HATIMA YA WANARUANGWA

    February 11, 2026
  • NGUVU YA HAZINA YA MADINI INAYOBADILI HATIMA YA WANARUANGWA

    February 11, 2026
  • ASHALONGO FC VS KIBWANA FARM FC, HAKUNA MBABE

    February 08, 2026
  • RAS LINDI AWAHIMIZA MAAFISA HABARI KUIMARISHA UHUSIANO NA VYOMBO VYA HABARI

    February 05, 2026
  • Ona zote

Video

MAENDELEO YATAKUJA KWA KULIPA USHURU, TOZO NA ADA ZA HALMASHAURI. MWANANCHI LI0A KODI KWA MAENDELEO YETU
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • Mpango wa Bajeti 2017/2018(MTEF)
  • Watumishi Portal

Kurasa zinazofanana

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • BARAZA LA MITIHANI

Idadi ya Wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Mahali

Anuani zetu

    Ruangwa

    Anuani ya Posta: S.L.P 51

    Simu ya Mkononi: 0732932312

    simu: 0732932312

    Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera za Usiri
    • Kanusho
    • Maswali na Majibu
    • Ramani ya Eneo
    • Huduma

Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa