Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Mhe. Hassan Ngoma amefanya ziara ya kutembelea Kata ya Nkowe leo Septemba 27, 2024 ikiwa ni muendelezo wa ziara ya kusikiliza kero za wananchi wa Wilaya ya Ruangwa
Katika ziara hiyo ameambatana na wakuu wa Idara mbalimbali ikiwemo ya Idara ya Elimu, TANESCO, RUWASA, Kamati ya Ulinzi na Usalama, na nyinginezo kwa lengo la kujibu kero za wananchi
Katika sekta ya Elimu Kata hiyo imekuwa na changamoto ya madarasa katika shule ya msingi Kipindimbi ambapo Afisa elimu wa Wilaya Ndugu. Philipo Siyaya ameeleza uwepo wa bajeti ya BOOST ambayo itatumika kurekebisha madarasa hayo
Aidha, DC Ngoma amesema kuwa fedha za Boost zitumike vizuri ili kuhakikisha madarasa hayo yanakamilika na watoto wanasomea sehemu nzuri
Katika hatua nyingine, Mhe. Ngoma amesisitiza wazazi kupeleka chakula shuleni kwani atayeshindwa kupeleka mpaka mwisho wa mwezi huu wa Septemba atachukuliwa hatua za kisheria
Kwa upande wake, Kaimu Maneja wa TANESCO Ndugu Wakati George amewataka wananchi kuvuta umeme katika nyumba zao na kuacha kulalamikia nguzo za umeme
Akifafanua suala hilo DC Ngoma amewaleza wananchi kutumia nafasi hiyo kwani bei ya kuvuta umeme ni shilingi 27000 ambayo kila mtu anaweza kuilipa
Mbali na hayo, Katika suala la changamoto ya maji Kaimu Meneja wa RUWASA amewapa imani wananchi kuhusu mradi wa maji wa Nyangao unagharimu kiasi cha sh. Bilioni 119 ambao unatarajiwa kuwafikia wananchi mwanzoni mwa mwaka ujao
Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa amehitimisha mkutano huo kwa kuwasihi wananchi kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa ili kuchagua viongozi bora watakao waletea maendeleo katika maeneo yao.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa