Wakazi wa Kata ya Likuja kijiji cha Mpara wameiomba Serikali kuendelea kuwapatia adhabu kali wale wanaowakatisha masomo watoto wakike kwa kuwapatia ujauzito au kuwaoa huku ni wanafunzi.
Hayo yamesemwa wakati wa Mdahalo wa kijiji ulioendeshwa na Chama cha Wanahabari wanawake Tanzania(TAMWA) leo Aprili 1/2019
ombi hilo limetokana na kukithiri kwa watoto waliopata ujauzito wakiwa shule au kukakata kuendelea na masomo kutokana na kurubuniwa na vijana.
Naye mkazi wa kitongoji cha Mgomba Mshamu Malibiche amesema kitendo cha watoto wa kike kufeli na kupata ujauzito wakiwa shule kimekithiri katika maeneo hayo kutokana na kuwa na hali ya wanaoharibu wanafunzi hao kutokupata adhabu wanayositahiki
Amesema tatizo ni Wazazi wa mabinti wanaopata ujauzito kwani inapotokea kijana wao amepata mimba wao wanapewa rushwa kutoka kwenye familia ya mzazi wa kiume hali inayopelekea kutoka kupatikana kwa ushahidi.
"Wazazi tuamke sasa tuwasaidie watoto wetu wakike tuwalinda ili wapate elimu iliyobora na katika mazingira salama tuisaidie serikali kufichua waharibifu wa watoto wetu" amesema Malibiche.
Vile vile Bi Arafa Mohammed amesema tatizo la ndoa za utotoni litaweza kumalizwa endepo mashekhe wanaoozesha wakiwekewa sheria inayompasa kabla ya kuozesha afuatilie kama mtoto huyo ni mwanafunzi au la na je umri wake ni zaidi ya miaka 18 na atakapokiuka achukuliwe hatua za kisheria.
Pia aliuomba uongozi wa Wilaya kuwachukulia hatua wazazi wa kiume wanaokata kutoa huduma kwa watoto wao hali inayopelekea mtoto kukosa huduma bora na elimu kwasababu ya baba kutomuhudumia.
wakati huo huo Mtendaji wa kata ya Likunja Athman Abdallah aliushukuru uongozi wa TAMWA kwa kuwapatia wakazi wa kata ya Likunja elimu ya kupinga ukatili wa kijinsia kwa mtoto wa kike na wanawake.
Pia ametoa wito kwa wakazi wa kata ya Likunja kushirikiana naye kufichua wale wanaoharibia wanafunzi masomo yao, amesema hatofumbia macho mtu yoyote atakaebaini amefanya uharibifu huo.
"muache asome tumsaidie mtoto wakike afikie malengo yake nikikubaini sitokuacha salama na nikibaini mzazi mtoto wako amepewa ujauzito au anaishi na mwanaume huku ni mwanafunzi alafu ujachukua hatua yoyote nitaanza nawewe na mtoto wa mwenzio naye ni wako pia" amesema Mtendaji
Aidha amewataka wakazi wa kata hiyo kuzingatia makubaliano na sheria wanazowekeana, na kuwakumbusha marufuku matumizi ya pombe wakati wa kazi na atakaemkamata anauza au anakunywa atamchukulia hatua kali za kisheria.
(Mwisho)
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa