• Anuani zetu |
    • Maswali na Majibu |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Ruangwa District Council
Ruangwa District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Uongozi wa Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Ardhi
      • Elimu Msingi
      • Afya
      • Maji
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Fedha na Biashara
      • Elimu Sekondari
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Usafi na Mazingira
      • Kata
    • Vitengo
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Ugavi
      • Nyuki
      • Sheria
      • Uchaguzi
      • Tehama
    • Kata
      • Nandagala
      • Mbekenyera
      • Likunja
      • Mnacho
        • Nangumbu
      • Malolo
      • Nachingwea
      • Ruangwa
      • Makanjiro
      • Mbwemkuru
      • Narungombe
      • Nangumbu
      • Luchelegwa
      • Chinongwa
      • Mandawa
      • Chunyu
      • Matambarale
      • Nkowe
      • Nambilanje
      • Nanganga
      • Namichiga
      • Mandarawe
      • Chibula
      • Chienjele
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Madini
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za Kudumu
    • Ratiba
  • Mradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi ya Afya
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Videos
    • Hutuba
    • Albamu ya Picha
    • Habari
    • Tukio
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari

Msiwanyanyapae wagonjwa wa Ukimwi- Ngoma

Posted on: December 1st, 2021

Mkuu wa wilaya ya Ruangwa Mhe. Hassan Ngoma amewataka wananchi kuacha mara moja tabia ya kuwanyanyapa waathirika wa ugonjwa wa ukimwi kwa sababu ugonjwa huo hautokani na matakwa ya kibinadamu.

Mhe. Ngoma amesema hayo wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya ukimwi kitaifa yaliyofanyika kiwilaya kijiji cha Chinokolo leo 01/12/2021 ambapo amesema kuwa hakuna anayeweza  kupata maambukizi ya virusi vya ukimwi kwa kukaa na mtu sehemu moja, kula pamoja au kushirikiana naye katika kufanya kazi za kuongeza kipato.

“Msiwanyayapae waathirika Huwezi kupata maambukizi kwa kushikana mikono na mtu watu wenye maambukizi  wanahaki kama walivyo wasio na maambukizi" Amesema Mhe. Ngoma.

Aidha amebainisha kuwa  ni muhimu watu kuendelea kuchukua tahadhari kwa  kujikinga na kuwakinga wengine kwani ukimwi upo na unaua.

“Kumekuwa na kauli za Ukimwi ni ugonjwa wa kawaida kama yalivvyo malaria au mafua kauli hizi zinachochea maambukizi nawakumbusha ukimwi upo jaman na unatisha tuache kuchukulia poa mlinde na mkinge umpendae na ukimwi haupimwi kwa macho usimuone mtu

amenona ukaona huyu anakufaa bila kupima huwezi jua huyu anakufaa au la acheni kuangalia kwa macho macho si kipimo sahihi kipo kipimo sahihi nendeni kwenye zahanati zenu mkapime” Amesema Mhe. Ngoma

Mhe.  Ngoma amesisiziza watoto ambao ni yatima na wamepata maambukizi kutoka kwa wazazi wao na kwa sasa wanaishi na watu wengine wahamasishwe kwenda kuchukua dawa kwa wakati.

Katika hatua nyingine Mhe. Ngoma amewataka wananchi kutoa ushirikiano wa kutosha kwa maafisa watakaokuwa wanafanya sensa ya watu na makazi ambayo inatarajiwa kuanza mwakani mwezi Agosti.

Pia amewataka wananchi kuendelea kujikinga na ugonjwa wa corona na kuendelea kufuata masharti yote yaliyowekwa na kwenda kupata chanjo kama inavyoelekezwa na serikali.

“Acheni kusikiliza maneno ambayo hayana ukweli ndani yake kuwa ukichanjwa unapata madhara baadae nendeni mkapate chanjo ili mzidi kujikinga” Amesema Mhe.Ngoma.

Kwa upande wake  Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Mhe. Mikidadi Mbute ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudhibiti Ukimwi amewataka waganga wa kienyeji kutoa tiba zao kwa kufuata utaratibu na si kuwarundika wananchi katika eneo moja.

Mhe. Mbute amesema Kuna baadhi ya waganga wanatabia za kutoa tiba kwa kuweka watu wengi katika maeneo yao na kutoa dawa kwa vifaa ambavyo wanatumia mtu zaidi ya mmoja jambo linaloweza kusababisha mlipuko wa magonjwa na ongezeko la maambukizi ya virusi vya Ukimwi.

“Mganga mkuu fanya kupita katika hayo maeneo uone mtoe elimu kwa watoa tiba na wapokea tiba ili tuweze kupunguza kasi ya maambukizi katika wilaya yetu”  Amesisitiza Mhe. Mbute.

Kilele cha Maadhimisho ya siku ukimwi duniani kimefanyika kiwilaya katika kata ya Makanjiro kijiji cha Chinokole huku  kauli mbiu ya maadhimisho hayo kwa mwaka huu ikiwa ni "Zingatia usawa tokomeza ukimwi tokomeza magonjwa ya mlipuko".


MWISHO

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI HALMASHAURI YA WILAYA YA RUANGWA November 08, 2023
  • TANGAZO LA NAFASI ZA WAHUDUMU WA AFYA 872 KWA NGAZI YA JAMII HALMASHAURI YA WILAYA YA RUANGWA July 09, 2024
  • TANGAZO LA AJIRA HALMASHAURI YA WILAYA YA RUANGWA August 01, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA RUANGWA March 13, 2023
  • Ona zote

Habari mpya

  • MKURUGENZI WA RUANGWA AHIMIZA USAFI NA MAZOEZI KWA AJILI YA AFYA BORA

    May 10, 2025
  • SMAUJATA YAENDESHA ELIMU DHIDI YA UKATILI WA KIJINSIA KWA WASICHANA RUANGWA

    May 09, 2025
  • BURIANI

    May 07, 2025
  • MHE. MAJALIWA AAINISHA MAFANIKIO MAKUBWA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO RUANGWA CHINI YA UONGOZI WA RAIS SAMIA

    May 03, 2025
  • Ona zote

Video

MAENDELEO YATAKUJA KWA KULIPA USHURU, TOZO NA ADA ZA HALMASHAURI. MWANANCHI LI0A KODI KWA MAENDELEO YETU
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • Mpango wa Bajeti 2017/2018(MTEF)

Kurasa zinazofanana

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • BARAZA LA MITIHANI

Idadi ya Wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Mahali

Anuani zetu

    Ruangwa

    Anuani ya Posta: S.L.P 51

    Simu ya Mkononi: 0732932312

    simu: 0732932312

    Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera za Usiri
    • Kanusho
    • Maswali na Majibu
    • Ramani ya Eneo
    • Huduma

Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa