Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka wakulima wa ufuta katika mikoa inayolima zao hilo nchini kuuza kwa kutumia njia ya minada na si mashambani.
Ametoa agizo hilo leo Machi 03, 2018 wakati akizungumza kwa nyakati tofauti na wananchi wa vijiji vya Nachiungo,Narungombe na Chikwale, Wakati wa Ziara yake ya Kikazi Wilayani Ruangwa.
“Waziri Mkuu ambaye yuko wilayani Ruangwa kwa ziara ya kikazi amesema ili wakulima waweze kupata tija ni vema wakauza ufuta wao kwa kupitia minada kama inavyofanyika katika zao la korosho”
“Usikubali kumuuzia mtu yeyote ufuta wako ukiwa shambani kwasababu bei atakayo nunulia ni ndogo kulinganisha na sokoni, naamini ufuta wote ukiuzwa katika minada mtaona faida mnachotakiwa ni kuwa wavumilivu mnapovuna msikubali kuuza mashambani.” Amesema Waziri Mkuu
Kufuatia agizo hilo amemuagiza Mkurungenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa, Bw. Andrea Chezue aandae utaratibu wa maeneo ya kuandalia ufuta na kufanyia minada.
Amesema ufuta unaolimwa nchini ni bora na unapendwa sana duniani hivyo wasiwe na wasiwasi. Mikoa Baadhi inayolima ufuta kwa wingi ni Lindi,Pwani,Dodoma,Manyara,Kigoma na Singida.
Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amesema vijiji vyote visivyokuwa na umeme nchini vikiwemo vya wilaya ya Ruangwa vitaunganishiwa katika REA awamu ya tatu.
Amesema wananchi waendelee kuwa na subira kwasababu tayari mkandarasi ameshaanza kazi ya kuunganisha umeme katika vijiji vingine vya wilaya hiyo na atafika kwenye maeneo yao.
Alibainisha kuwa mkakati wa raisi Dkt.John Magufuli ni kuhakikisha wananchi wote nchini waunganishiwa nishati ya umeme kwenye majumba yao,hivyo waendelee kuwa na subira na kushirikiana na serikali yao.
Kuhusu suala la upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama alisema”Huduma ya upatikanaji wa maji safi na salama kwa wananchi ni miongoni mwa vipaumbele vya serekali ya awamu ya Tano, hivyo vijiji vyote vitapata maji”.
Pia alitumia fursa hiyo kuwahamasisha Wananchi kote nchini kutunza vyanzo vya maji ili kuliepusha Taifa kugeuka jangwa pia miradi inayoletwa na serekali iwe endelevu.
“Acheni kufanya kilimo holela cha kuchafua mazingira kwa kulima mwaka huu shamba hili mwakani shamba lingine, serikali ya Vijiji vilivyo katika anzeni utaratibu wa kuzuia watu kulima kilimo cha kuhama hama ili kutunza vyanzo vya maji vilivyopo Wilayani Ruangwa” Amesema Waziri Mkuu
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa