Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Ruangwa Mwl. George Mbesigwe leo Agosti 21, 2025 amemkabidhi fomu ya kugombea nafasi ya Ubunge Mgombea wa Chama cha ACT Wazalendo, Joachim Gerion Ng’ombo, katika Ofisi za Uchaguzi za Jimbo hilo zilizopo kwenye Ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa.
Ng’ombo amewasili katika ofisi hizo akiwa ameambatana na viongozi pamoja na wanachama wa chama chake, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kushiriki katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, mwaka huu.
Aidha, kwa mujibu wa ratiba ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), uchukuaji na urejeshaji wa fomu za wagombea unaendelea hadi Agosti 27, kabla ya uteuzi rasmi wa majina ya watakaopitishwa kuwania nafasi mbalimbali za uongozi.
Vilevile, mchakato wa kugombea nafasi za Ubunge na Udiwani unafanyika katika majimbo yote ya uchaguzi nchini kwa kuzingatia kanuni na taratibu zilizowekwa na INEC.
Kwa upande mwingine, wagombea na vyama vya siasa vimetakiwa kuhakikisha vinakamilisha masharti yote ya kisheria na kikanuni ili kuepuka changamoto wakati wa hatua ya uteuzi na kampeni.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa