Wasimamizi Wakuu na Wasaidizi wa Uchaguzi Mkuu waaswa kuwa waadilifu na wasikivu ili kuweza kufanya uchaguzi wenye amani.
Hayo yamesemwa Leo tarehe 25/10/2020 na Msimamizi Mkuu wa Uchaguzi Jimbo la Ruangwa Frank Chonya wakati anafanya ufunguzi wa mafunzo ya siku mbili ya wasimamizi wa vituo vya kupigia kura wilayani Ruangwa.
Pia amesema lengo la mafunzo hayo ni kujifunza namna ya kufanikisha uchaguzi mkuu,kukabiliana na changamoto za uchaguzi kwa kufuata sheria kanuni zilizowekwa na tume ya uchaguzi NEC
Hata hivyo wasimamizi wote wameweza kula kiapo cha kutunza siri pamoja na kujiondoa uanachama wa chama chochote ili kuweza kutekeleza majukumu yao bila kufungamana na itikadi ya chama chochote kile na kutunza siri za uchaguzi ili kuweza kudumisha amani iliyokuwepo katika nchi ya Tanzania
Aidha jumla ya wasimamizi waliopatiwa elimu ni jumla ya 1,037 ambao wamegawanyika katika vituo mbalimbali vya mafunzo ikiwa hawa mchopa,wasimamizi wa kata Nangumbu,Nanganga,Chinongwe,Malolo na Luchelegwa Lucas maria wasimamizi kata Likunja,Chienjele,Mnacho Nandagala na Nkowe Ruangwa secondary wasimamizi kata ya
Mandarawe,Mbekenyera,Matambarare,Namichiga,Chibula,Mandarawe na Nambilanje kituo cha kanisani wasimamizi kata za Ruangwa,Nachingwea,Chunyu,na Narungombe.
Mafunzo haya yanafanyika ili kuweza kuwawezesha wasimamizi kuwajibika kwa ufasaha katika uchaguzi Mkuu wa Rais ,Mbunge pamoja na madiwani unaotarajiwa kufanyika oktober 28/2020.
MWISHO
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa